Habari za Punde

Bwejuu Dongwe waunda kamati kushughulikia changamoto zao

Waakazi wa shehia ya Bwejuu Dongwe wameunda kamati yakufuatia tatizo la maji katika ofisi ya Halmashauri ya wilaya kusini ili kulipatia ufumbuzi tatizo hilo ambalo linaonekana ni changamoto.

Wakizungumza na Gazeti la Zanzibar Leo, Mkaazi wa Bwejuu Dongwe, Chum Haji Ali (58) amesema baada kuhamasika na elimu walioipata kupitia Mradi wa Kukuza Uwajibikaji (PAZA) wananchi wa eneo hilo wameona waunde kamati ili kufuatilia kwa ukaribu suala la upatikanaji wa maji lakini bado tatizo hilo  limeshindikana mpaka sasa.



Kufuatilia kushindikana kupatiwa ufumbuzi changamoto hiyo wananchi hao wamewaomba Chama Cha Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA-ZANZIBAR) kuendeleza Mradi wa kukuza Uwajibikaji Zanzibar  ili waweze kufuatilia matatizo yao kwa ukaribu.

“Kutokana na tatizo la maji safi na salama bado halijatatuliwa katika shehia ya Bwejuu Dingwe basi tunawaomba TAMWA waendeleze huu mradi kwani umetusaidia katika kutupa elimu ya wananchi wengi wamenufaika nao kwa kupata elimu ya kujua haki zetu na namna ya kuzidai” alisema Chum.


Amesema Maafisa wa maji katika ofisi hiyo wamesema suali la maji watalifuatilia katika ofisi ya Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) lakini hadi sasa hakuna dalili za upatikanaji wa maji katika eneo hilo.

Pia amesema tatizo la kuingiliwa na maji taka katika eneo hospital  na skuli ya Bwejuu Dongwe bado linaendelea ndio maana wameomba Mradi wa PAZA undelee ili uweze kutatua changamoto hizo zilikua bado hajatatuliwa katika eneo lao.

Aidha amesema huduma ya afya imeimarika kwa kuletewa madaktari na vifaa vya kutibiwa wagonjwa hali ambayo imewandolea usumbufu  wananchi wa  Bwejuu dongwe ambapo awali walikuwa wakipata shida.

Pia amesema huduma ya wazazi kujifungua wamepewa maelekezo wazazi wakajifungulie katika hospitali ya Jambiani.

Kwa upande wa elimu amesema banda moja la skuli limefanyiwa ukarabati hivyo wanashukuru Mradi wa PAZA umehamasisha watu kujua utaratibu wa kwenda ofisi ya Halmashauri kufuatilia changamoto zinazowakabili na namna ya kuzidai.

“Jambo la kufurahisha kwenye mradi huu wananchi wamehamasika lakini ile kujua haki zao na wapi wakadai haki zao pia ni jambo la kushukuru sana maana zamani shida zetu tulikuwa hatujui tukazipeleke wapi, lakini sasa tumejua” amesema.


Kwa upande wake Afisa Maji wa Wilaya ya Kusini, Bw Hafidh Hassan Mwinyi amesema Baadhi ya shehia ya Bwejuu wanapata maji  na baadhi ya maeneo huwa hawapati maji.

Bwana Hafidh amesema eneo la Mbwejuu Dongwe eneo hilo halipati maji kutokana na kuwa kuna mwinuko wa ardhi ndio imepelekea waakaazi wa eneo hilo kukosa maji safi na salama.

“Ni kweli tuna hiyo changamoto ya baadhi ya maeneo kukosa maji lakini hili tatizo linafanyiwa kazi ninachoweza kuahidi ni kuwaambia wananchi wavumilie na wavute subra wakati mipango ya kurekebisha na kuwatengenezea ili wapate maji ikifanywa” aliahidi Afisa huyo wa Maji Wilaya


Amesema hatua za ufumbuzi zinaendelea kushughulikwa na Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) hivyo amewaomba wananchi waendelee kustahamili huduma ya maji safi na salama itapatikana taratibu zikishakamilika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.