NA K-VIS BLOG/Khalfan Said.
MITAMBO
ya kufua umeme wa gesi asilia kwenye kituo cha Kinyerezi II jijini Dar es
Salaam imetumia teknolojia ya kisasa kabisa ijulikanayom kama combine cycle na kuwa nchi ya kwanza
Afrika Mashariki kutumia teknolojia hiyo. Akifafanua
kuhusu teknolojia hiyo, Meneja Miradi (uzalishaji) wa Shirika la Umeme Nchini
TANESCO, Mhandisi Stephene S. A. Manda, amesema baada ya mitambo ya kufua umeme
utokanao na gesi, mvuke unaozalishwa kwa awamu ya kwanza kutokana na joto
hupelekwa tena kwenye mtambo mwingine na huko unazalisha umeme wa awamu ya pili. Alisema,
tayari TANESCO imepokea maombi kutoka nchi mbalimbali zikiwemo zile za SADC
kuja kujifunza teknolojia hiyo, ambapo katika mitambo nane ya kufua umeme
iliyoko Kinyerezi II, miwili ni ile itokanayo na mvuke (steam turbines) “Tulivyokuwa
na mkutano wa SAPP kule Arusha yaani Southern
Africa Power Pool nchi mbalimbali zimeonyesha nia ya kuja kujifunza
teknolojia hii.” Alisema. Mhandisi
Manda ametoa wito kwa vyuo mbalimbali vinavyotoa taaluma ya uhandisi wa umeme
kupeleka wanafunzi ili wajifunze teknolojia hiyo ya kisasa. “Wanafunzi
wanao….Practice engineering wako
kwenye field ambao hawajaona
teknolojia inavyofanya kazi waje wajifunze.” Alisema.
Moja ya mitambo ya kufua umeme utokanao na mvuke (steam turbine) kwenye kituo cha kufua umeme wa gesi asilia Kinyerezi II jijini Dar es Salaam.
Meneja Miradi (uzalishaji) wa Shirika la Umeme Nchini
TANESCO, Mhandisi Stephene S. A. (kulia) na Meneja wa kituo cha kufua umeme wa gesi cha Kinyerezi II, Mhandisi Ambakisye Mbangula, (katikati), wakimsikiliza mhandisi huyu kutoka nje anayehudumu kwenye mitambo hiyo wakati huu wa kumalizia ujenzi.
Mhandisi Manda akifafanua kuhusu mitambo ya kisasa iliyofungwa kwenye kituo hicho.
Mhandisi Manda akizungumza na wafanyakazi wa TANESCO kwenye chumba cha udhibiti mwenendo wa mitambo ya umeme (control room) Kinyerezi II.
No comments:
Post a Comment