Habari za Punde

Wananchi wa Kijiji Cha Kikungwi Wilaya ya Kati Unguja Wafurahia Huduma Zinazotolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


Na Mwajuma Juma, Zanzibar


WANANCHI wa kijiji cha Kikungwi Wilaya ya Kati Unguja wamefurahiya na uduma mbali mbali wanazozipata ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiwapa matumaini makubwa na Serikali zao.
Akuzungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho Bahati Issa alisema kuwa katika kijiji chao wanashukuru kuona huduma nyingi wanaziapata ikiwemo suala la elimu, afya na changamoto kubwa ambayo mpaka sasa wamebakia nayo ni kuhusu maji.

Alifahamisha kwamba hivi karibuni kulitokea changamoto moja tu lakini kwa upande wa madaktari wapo vizuri na wamejitahidi kwani wamekuwa wakipata huduma nzuri.

Hata hivyo alisema kuwa kupitia Mradi wa Kukuza Uwajibikaji Zanzibar PAZA wamekuwa na upeo mkubwa wa kuweza kufatilia haki zao ambazo awali walikuwa hawazitambui.

Kwa upande wake Kassim Makame Ali Kombo amesema kuwa bado miundo mbinu
ya maji inahitajika kwa sababu bomba za awali ambazo zilikuwepo ni mbovu.

Alisema kuwa kumekuwa na  hatua mbali mbali zimechukuliwa  zimepiga hatua nzuri na kuleta matumaini kwa wakaazi wa kijiji hicho katika upatikanaji wa maji.

“Kuna mafanikio makubwa katika mradi huu, umetusaidia vya kutosha sasa changamoto ambayo tunayo ni maji nah ii tayati tumekuwa na mazungumzo mazuri na viongozi wa Halmashauri wa wilaya yetu nadhani nayo itaondoka”, alisema.

Hata hivyo alisema kuwa pamoja na kwamba mradi huu umemalizika lakini inabidi waendelee kushirikiana ili kuhakikisha vijiji vyao vinakuwa na maendeleo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.