Habari za Punde

Longido Yaendelsha Msako wa Kuwakamata Wazazi Wasiowapeleka Shule Watoto Wao.

Katibu tawala akimkaribisha mkuu wa wilaya hiyo kuongea na wadau wa elimu kwenye maadhimisho ya siku ya taaluma jana wilayani Longido picha na Mahmoud Ahmad Longido
Mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe akiongea na wadau wa elimu wilayani humo kwenye kilele cha siku ya Taaluma iliyofanyika kiwilaya kwenye ukumbi wa halmashauri jana picha na Mahmoud Ahmad Longido.
Waalimu na wadau mbalimbali wa elimu wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya hiyo Frank Mwaisumbe mwenye shati jeusi katikati wakati akitoa hotuba yake kwenye sherehe za siku ya Taaluma kiwilaya jana wilayani Longido picha na Mahmoud Ahmad Longido.
Na Ahmed Mahmoud Longido
Wilaya ya Longido imejipanga kuendesha Msako wa kuwakamata wazazi ambao hawajawaandikisha watoto wao shuleni kwani kwa kufanya hivyo wanavunja sheria ya elimu na sheria ya watoto kutokana na idadi ndogo ya watoto wanaoandikishwa katika shule mbalimbali jambo ambalo linawasukuma kufanya msako huo.
Mkuu wa Wilaya ya Longido  Frank James akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Elimu ,amesema kuwa  msako huo ambao utafanyika majumbani na iwapo watabaini kuna wanafunzi hawajaandikishwa watawachukulia hatua ikiwemo kuwakamata na kuwafungulia mashtaka kwa kuwanyima watoto haki ya kupata elimu.
Aidha amesema kuwa msako huo utahusisha maeneo ya malisho kwani wafugaji wengi hawapendi kuwaandikisha watoto ili waweze kuwatumia watoto kuchunga mifugo yao badala ya kwenda shule jambo ambalo serikali haitalifumbia macho.
Ametanabaisha kuwa uwepo wa asilimia ambazo wilaya ilijiwekea hauwiani na watoto walioandikishwa kuingia Darasani wilayani huo ambapo 56 asilimia pekee ndio walioandikishwa kuingia darasa la kwanza ambapo wa kidato cha kwanza ni asilimia 32 hii imetufanya kuanza kwa msako wa nyumba kwa nyumba na atakayebainika kuwaficha watoto tutamchukulia hatua kali.
“Niwaombe wadau wa elimu na wazazi kuwapeleka watoto shule kabla msako haujaanza rasmi tena kwa hiyari yao kwani tukimkuta motto anachunga mifugo yeye na mifugo yake tutawakamata na mzazi au mlezi hatua kali tutachukuwa kwa hili hatutamvumilia yeyote” alisisitiza Mwaisumbe
Afisa Elimu shule ya Msingi Wilaya ya Longido Natang`aduaki Mollel amesema kuwa wilaya hiyo imefanya vizuri katika mitihani ya kitaifa licha ya changamoto ya utoro,ndoa za utotoni na umbali mrefu wa kufika mashuleni hivyo wataweka mikakati thabiti kuhakikisha kuwa wanafanya vizuri kila mara.
Amesema kuwa mikakati ya wilaya hiyo ni kuondokana na mapungufu mbali mbali yanayoikabili jamii kupata elimu kwa kushirikiana na wazazi na walezi kuhakikisha elimu wilayani humo inapewa kipaumbele cha kwanza ikiwemo kuwapeleka watoto shule na waalimu kutimiza wajibu wao ili kuipaisha wilaya hiyo.
Niwasihi sana wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha elimu wilayani hapa inazidi kupaa na kushika nafasi za juu tusione tumefanikiwa bado ni safari ndefu ya kufikia mafanikio tunaohitaji ni ushirikiano pekee na kutimiza wajibu ndio vitatufanya kufanikiwa”alisema Mollel
Kwa upande wao Walimu Ephata Mwalimu Mkuu shule ya msingi Longido..na Sabato Petro Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngarnaibor waliotoka katika shule za Msingi na sekondari zilizofanya vizuri wamesema kuwa ushirikiano mzuri kati ya wazazi,walimu na Viongozi wa kiserikali umesaidia kuleta tija na kuwafanya watoto wasome kwa bidii

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.