Habari za Punde

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Azungumza na Viongozi na Wanachama wa CCM Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja leo Akiwa Katika Ziara Yake Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wanachama wa CCM Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati wa ziara yake leo katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, kutembelea Miradi ya Maendeleo.

Na.Abdi Shamnah.Ikulu Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,azungumza na Viongozi wa Kamati ya siasa ya CCM Wilaya Kaskazini ‘A’, Viongozi wa ngazi mbali na wanachama wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Kaskazi A Unguja leo.
Alisema Wilaya hiyo ni miongoni mwa zile zenye changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi, inayochangiwa na wananchi pamoja na baadhi ya  viongozi, wakati wa mkutano wake uliofanyika ukumbi wa hoteli ya Lagema Nungwi.
Aliwataka wale wote wenye tabia hiyo kuacha vitendo hivyo, akibainisha kuwa vina athari kubwa katika ustawi wa sekta ya Utalii nchini.
Aidha, Dk. Shein aliwataka wanachama wa chama hicho kujipanga vilivyo kwa ajili ya uchaguzi  mkuu ujao wa 2020, sambamba na viongozi wa majimbo (Wabunge na Wawakilishi) kutumia kipindi kilichobaki kabla ya uchaguzi huo kutekeleza ahadi walizoweka kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.