Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Balozi Mdogo wa India Zanzibar.

Balozi Mdogo wa India liyepo Zanzibar bwana T.C. Barual akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kabla ya mazungumzo yao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiishukuru Serikali ya India kupitia kwa Balozi Wake Mdogo Bwana Barual kwa jitihada za kuunga mkono harakati za Maendeleo ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, akisisitiza jambo wakati akizungumza na Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana Barual Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana Barual akimuhakikishia Balozi Seif India kuendelea kushirikiana na Zanzibar katika kudumisha Uhusiano wa Kidiplomasia.

Picha na –OMPR – ZNZ.

Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana kwa mazungumzo na Balozi Mdogo ya India aliyepo Zanzibar Bwana T C. Barual ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Katika mazungumzo yao Balozi Seif ameishukuru na kuipongeza Serikai ya India kwa jitihada zake za kusaidia harakati za Maendeleo ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Balozi Seif alisema miradi ya Maji safi na Salama inayoendelea kuwekewa miundombinu wakati huo ndani ya Mkoa wa Mjini Magharibi kwa kuungwa mkono ya Serikali ya India, huduma za Afya, Elimu na Kilimo imeleta ustawi kwa Wananchi walio wqengi Visiwani Zanzibar.
Alitolea mfano wa Sekta ya Afya ilivyoongeza chachu ya uhusiano na Ushirikiano kati ya Zanzibar na India ambapo idadi kubwa Wagonjwa wa Zanzibar wamekuwa wakipata huduma za Afya katika Hospitali tofauti Nchini India.
Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuomba UbaloziMdogo wa India hapa Zanzibar kupitia Balozi wake kuandaa mpango Maalum wa kuwapatia Mafunzo Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na Maafisa wao.
Alisema Mpango huo endapo unaweza kusimama utawasaidia kuwajengea uwezo zaidi wa uwajibikaji Viongozi hao katika kuwatumikia vyema Wananchi katika misingi ya uwelewa mpana.
Naye Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana T.C. Barual alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba wazo lake litafanyiwa.
Alisema hatua hiyo itasaidia kuongeza kasi ya uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo baina ya India na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.