Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu
wa Rais Mhandisi Joseph Malongo (kushoto) akiendesha kikao kazi cha Makatibu
Wakuu kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimejadili juu
ya uratibu na ufuatiliaji wa masuala ya Muungano. Kulia ni Bw. Abdallah Mitawi Kaimu Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ambae ni Mwenyekiti Mwenza. Kikao hicho
kimefanyika hii leo katika Ukumbi wa Hazina, Jijini Dodoma.
Sehemu ya Wajumbe wa kikao
hicho ambao ni Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(SMT) wakifuatilia kikao hicho. Jumla ya Makatibu Wakuu 26 kutoka Tanzania Bara
wamehudhuria kikao hicho.
Sehemu ya Wajumbe wa kikao
hicho ambao ni Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)
wakifuatilia kikao hicho, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.
Jumla ya Makatibu Wakuu 13 kutoka Zanzibar wamehudhuria ikiwa ni maandalizi ya
kikao cha Kamati ya pamoja kitakachofanyika siku ya kesho Mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment