Habari za Punde

Skuli ya Elimu Endelezi na Utaalamu ya SUZA Yatoa Zawadi Kwa Washindi wa Bonaza la IT.

Mkuu wa Skuli ya Elimu Endelevu na Utaalamu (SCOPE) ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar,  Dk. Haji Ali Haji akitoa maelezo ya Bonanza la IT linalofanyika kila mwaka katika sherehe za kuwazawadia wanafunzi waliofanya vizuri zaidi mwaka 2019 zilizofanyika Kempasi Vuga Mjini Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya Kusini Unguja Idrissa Kitwana akizungumza na wakufunzi na wanafunzi walioshiriki Bonanza la IT linaloandaliwa na Skuli ya Elimu Endelezi na Utaalamu ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar katika sherehe za kuwapa vyeti na zawadi wanafunzi waliofanya vizuri zaidi mwaka 2019.
Mkuu wa Wilaya Kusini Idrissa Kitwana akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa IT Essential, Bassim Said Salum katika sherehe za kuwapa zawadi washiriki waliofanya vizuri zaidi katika Bonanza la IT la mwaka 2019 katika sherehe zilizofanyika Kempasi ya SUZA Vuga Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya Kusini Unguja Idrissa Kitwana akimkabidhi zawadi ya Laptop mshindi wa kwanza wa Coputer Application, Ali Suleiman Ali katika Bonanza la IT 2019 linaloandaliwa na Skuli ya Elimu Endelezi na Utaalamu ya SUZA.
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Idrissa Kitwana akimkabidhi cheti na fedha taslim Aboubakar Abdalla Khamis  ambae ni mmoja wa washindi wa Bonanza la IT mwaka 2019 katika sherehehe zilizofanyika Kempasi ya Vuga Mjini Zanzibar (kushoto) Naibu Makamu Mkuu wa UZA Fedha na Mipango Dk. Haroun Ali.
Baadhi ya wanafunzi walishriki Bonanza la IT linaloandaliwa na Skuli ya Elimu Endelezi na Utaalamu ya (SCOPE) ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar wakifuatilia sherehe za kutunukiwa vyeti na zawadi wanafunzi waliofanya vizuri zaidi mwaka 2019 zilizofanyika Kempasi ya Vuga Mjini Zanzibar.



Na Ramadhani Ali – Maelezo                                  9.2.2019
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Idrissa Kitwana amewataka vijana kuitumia fursa ya kuwepo Skuli ya Elimu Endelezi na Utaalamu (SCOPE) ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kujiendeleza katika masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliiano pamoja Lugha za Kigeni ili kujijengea mazingira mazuri ya ajira.
Alisema Skuli ya Elimu Endelezi na Utaalamu ya SUZA ni daraja muhimu kwa vijana wenye ndoto ya kuajiriwa katika taasisi mbali mbali ama kujiajiri wenyewe hivyo ni vyema kuitumia nafasi hiyo ambayo ni muhimu kwa maisha yao ya baadae.
Mkuu wa Wilaya alieleza hayo katika sherehe za kukabidhi vyeti na zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika Bonanza la IT la Skuli ya Elimu Endelezi na Utaalamu ya SUZA mwaka 2019 zilizofanyika Kempasi ya Vuga.
Alisema katika karne ya sasa ya 21 na karne zijayo, kuna umuhimu mkubwa kwa vijana kuwa na taaluma ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano pamoja na kuwa na uwezo wa kufahamu lugha nyingi za Kigeni hasa wakati huu ambapo Serikali inaelekeza nguvu za ajira kwenye sekta ya Utalii.
“Ujuzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano pamoja na Lugha za Kigeni ni mkombozi katika ajira za sekta ya Utalii na soko la pamoja la ajira kwa nchi za Afrika Mashariki,” alisisitiza Mkuu wa Wilaya ya Kusini.
Aliwashauri vijana ambao hawakubahatika kuingia elimu ya Sekundari ya juu na wale waliochaguliwa, pamoja na wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na binafsi kujiunga na Skuli ya Elimu Endelezi na Utaalamu ili kwenda na wakati wa sasa wa Sayansi na Teknlojia.
Mkuu wa Wilaya ya Kusini aliwataka Wafanyabiashara wa Zanzibar kuunga mkono juhudi za Skuli ya Elimu Endelezi na Utaalamu ya SUZA kwa kuwasaidia vijana kuinua vipaji vyao kwa kutoa motisha wa zawadi na kutangaza bidhaa zao kupitia mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka.
Akizungumza katika sherehe hizo, Mkuu wa Skuli ya Elimu Endeleza na Utaalamu ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar  Dk. Haji Ali Haji alisema malengo ya Skuli hiyo ni kuinua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi, vijana na jamii ya Zanzibar na Tanzania kwa jumla katika fani ya IT na kushajihisha wanafunzi kupenda fani hiyo.
Alisema hivi sasa SCOPE inaedesha programu nane za IT na mafunzo ya lugha ya Kifaransa, Kijerumani, Kiarabu na Kichina na hivi karibuni inampango wa wa kuanzisha lugha ya Kituruki na lugha ya Kiitaliano na itaongeza programu mpya nne za IT kuanzia mwaka huu 2019 hadi kufikia mwaka 2022 kwa ngazi ya cheti.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.