Habari za Punde

Waliofaulu Kidatu Cha Nne Stone Town International School Zanzibar Watakiwa Kuongeza Juhudi Kwani Safari Bado ni Ndefu Kwao.

Mwanafunzi Asia Juma Ali (kushoto) na Nathania Sleiman wakighani utenzi kwenye sherehe ya mahafali yakuwapongeza wanafunzi wa kitado cha nne waliomaliza Stone Town International School iliopo Kilimani Mjini Zanzibar mwaka jana.
Mjumbe wa Bodi ya Ushauri Tasisi ya Elimu Zanzibar Charles Lubega akielezea umuhimu wa elimu katika mahafali ya Stone Town International School pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi kuwahutubia wahitimu wa kidato cha nne na wanafuzi wanaoendelea na masomo.
 Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi Hamida Mussa Khamis akizungumza na wazazi na wanafunzi wa Stone Town International School ya Kilimani katika mahafali ya kidato cha nne ya skuli hiyo.
Katibu Tawala Mkoa Mjini Magharibi Hamida Mussa Khamis akimkabidhi cheti mwanafunzi Rahma Juma Juma mmoja kati ya wanafunzi wawili waliopata daraja la kwanza Skuli ya Stone Town International.
Mkurugenzi wa Stone Town International School Bi. Jamila Gulam Hussen akisoma hutuba katika mahafali ya kidato cha nne yaliyofanyika skulini kwao Kilimani Mjini Zanzibar.
Wahitimu wa Kidato cha Nne wa Stone Town International School wakiwa katika mahafali yao yaliowashirikisha pia wanafunzi wa darasa la sita yaliyofanyika skulini kwao Kilimani.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.