Habari za Punde

Uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Kituo Cha Afya Magirisi Jimbo la Kijitoupele Zanzibar, Wakati wa Ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Wilaya ya Magharibi B, Unguja.

Kituo cha Afya Magirisi  Jimbo la Kijitoupele Zanzibar, kilichojengwa na Mbunge na Mwakilishi na nguvu za Wananchi wa Jimbo hilo, kimewekwa Jiwe la Msingi leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Magharibi B, Unguja.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wa Vyama vya Siasa wakisubiri kumpokea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kuwasili ili kuweka Jiwe la Msingi Kituo cha Afya cha Magirisa Jimbo la Kijitoupele Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Mama Mwanamwema Shein, wakiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi Kituo cha Afya Magirisi Jimbo la Kijitoupele Zanzibar, akiwa katika ziara yake katika Wilaya ya Magharibi B,Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud, wakimsikiliza Daktari Dhamani wa Manispa ya Magharibi B, Unguja. Dkt. Rahma Abdallah Maisara, akitowa maelezo ya michoro ya ramani ya jengo hilo, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi lla Kituo cha Afya Magirisi leo. 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.