Habari za Punde

Upungufu wa mafuta wasababishwa na kuchelewa kwa Kampuni ya United Petroleum (UP) kuingiza mafuta kwa wakati

Na Mwashungi Tahir             Maelezo      
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar ZURA inapenda kuwajuilisha wananchi kwamba matatizo ya upungufu wa mafuta katika baadhi ya vituo iliyosababishwa na Kampuni ya United Petroleum (UP)kushindwa kuingiza mafuta  kwa wakati.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar ZURA Haji Kali Haji  huko ofisini kwao Maisara wakati alipokuwa akitoa taarifa ndogo  kuhusiana na upungufu wa mafuta.
Amesema ucheleweshaji huo wa kishindwa kuingiza mafuta kwa wakati kunatokana na kupeleka meli ya United Spirit 1 nchini Msumbiji  na kushindwa kuleta Mafuta Zanzibar kwa wakati hali ambayo imepelekea kupungua kwa mafuta ya Petroli katika baadhi ya vituo vya mafuta  hasa vituo vya Kampuni ya United Petroleum (UP).
Hata hivyo alieleza kwamba Kampuni ya Zanzibar Petroleum (ZP)  na Kampuni ya GAPCO  wameingiza mafuta nchini  na yanaendelea kusambazwa katika vituo vyao  vya mjini na vijijini kuanzia asubuhi ya leo .
Amesema hali halisi ya uwepo wa mafuta nchini kwa kila kampuni  ni kama ifuatavyo katika bohari kuu ya Mtoni leo Jumanne tarehe 5-3-209.
Kampuni ya GAPCO
*Petrol : Lita 942,317
*Diesal : Lita 799,629
*Kerosene : Lita 213,305
Kampuni ya ZANZIBAR PETROLEUM (ZP)
*Petrol : Lita 407, 415
*Diesel : Lita 904,688
*Kerosene : Lita 215,912
Kampuni ya UNITED PETROLEUM (UP)
*Petrol : Lita 98,152
*Diesel : Lita 205,505
*Kerosene: Lita 472,194
Aliendelea kusema jumla ya mafuta yaliopo  nchini kwa sasa ni kama ifuatavyo.
Petrol Lita 1,447,884 sawa na matumizi ya siku tisa (9)
Dizeli  Lita 1,909,822 sawa na matumizi ya siku kumi na mbili (12)
Mafuta ya Taa Lita 1,042,828 sawa na matumizi ya siku thalathini (30)
Pia alisema Kampuni ya United Petroleum (UP) inatarajia kuingiza mafuta kiasi cha tani 2.000 za Dizeli sawa na Lita 2,400,000 na Tani 1500 za Petroli  sawa na Lita 2,047,500 kwa kutumia meli mpya ya mafuta ya East Wind II siku ya Ijumaa ya tarehe 8-3-2019 ambayo yatamaliza kabisa tatizo la uhaba wa mafuta nchini .
Aidha aliendelea kusema Kampuni ya Zanzibar Petroleum (ZP) inatarajia kuingiza mafuta kiasi cha Lita 1,600,000 za Petroli kwa kutumia meli ya East Wind I siku ya Jumapili ya tarehe 10-03-2019.
Hivyo alisema ZURA imesikitishwa sana na hali ya uhaba mdogo wa mafuta uliojitokeza  hali ambayo imewasababishia wananchi kukosa huduma kwa kawaida.
Vile vile alieleza kwamba kutokana na hali hiyo ZURA imeyaagiza Makampuni ya Mafuta kuhakikisha kwamba yanasambaza mafuta kwa haraka na kurejesha huduma hiyo kwa wananchi na kuhakikisha inapatikana bila usumbufu.
Kwa hiyo ZURA inawaomba radhi wananchi wake kwa usumbufu uliojitokeza na kueleza kwamba inafuatilia kwa karibu matengenezo ya meli mbili zilizoharibika ili kuhakikisha hali ya upatikanaji wa mafuta nchini inarejea kama kawaida.
Akitoa wito Mkurugenzi Haji  alisema Mamlaka  inawasisitiza wananchi  kuacha tabia ya kusikiliza taarifa zisizo rasmin ambazo zinapelekea wananchi  kuwa na taharuki katika upatikanaji wa huduma hiyo.
Mwisho.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.