Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mama Asha Suleiman Iddi akimfariji mtoto Hassan Suleiman wakati alipowasili
Wilayani Muheza ambae ni mlemavu akiwa katika kigari chake maalum.
Vifaa mbali mbali vilivyotolewa katika
shughuli ya watoto wenye Mahitaji maalum
na wadau walioguswa na watoto hao, vifaa hivyo vinajumuisha baiskeli,
wll chair, pamoja na magongo kwa ajili ya kusaidia katika kutembea.
Mama
Tunu Pinda akimvisha Kofia Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi wakati akimzawadia
kupitia vifaa tofauti alivyovikabidhi kwa uongozi wa wilaya hiyo ikiwa ni
sehemu ya kuwachangia watoto hao. Mama Tunu Pinda ni mwenyekiti wa wake wa
viongozi Tanzania bara
Mama
Asha Suleiman Iddi Akimlisha Keki mtoto Maimuna Yahya wa skuli ya msingi ikiwa
ni moja ya kuwazawadia watoto waliofanya vizuri katika masomo yao.
Mke
wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman Iddi Akihutubia wananchi waliofika
katika zoezi la uchangiaji wa ujenzi wa mabweni ya Skuli ya Mlingano Sekondari
kwa wototo wenye Mahitaji maalum huko Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga
Mgeni Rasmi katika shughuli ya kuwachangia
watoto wenye mahitaji maalum Mama Asha
Suleiman Iddi akimkabidhi Mhe. Mkuu wa wilaya ya Muheza Eng. Asha Tumbo
Shillingi Million Sita (6,000,000/) kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya Wanafunzi
wenye ulemavu.
No comments:
Post a Comment