Habari za Punde

Mbunge wa jimbo la Kiembesamaki atoa misaada kwwa UVCCM wilaya ya Dimani kichama

 Mbunge wa Jimbo la Kiembesamaki Ibrahim Razza akivishwa skafu na Vijana wa UVCCM Wilaya ya Dimani Kichama, Nd.Hassan Mohammed (kulia) na Nd. Hamadi Ali walipotembelewa katika Tawi la CCM Kiembesamaki kwaajili ya kupatiwa misada  mbalimbali (Picha na Abdalla Omar).
  Katibu wa UVCCM Wilaya ya Dimani Kichama Ramadhan Abas Mcheju, akizungumza na kumuelezea changamoto zinazowakabili Vijana hao  (Picha na Abdalla Omar).
 Mbunge wa Jimbo la Kiembesamaki Ibrahim Razza akizungumza na Vijana wa UVCCM Wilaya ya Dimani Kichama, (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kuwapatia misaada mbalimbali katika ghafla iliofanyika Tawi la CCM Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi B Unguja (Picha na Abdalla Omar).
 Vijana wa UVCCM Wilaya ya Dimani Kichama,wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Kiembesamaki Ibrahim Razza (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kuwatembelea katika Tawi la CCM Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi B Unguja (Picha na Abdalla Omar).
 Mbunge wa Jimbo la Kiembesamaki Ibrahim akikabidhi msaada wa Kompyuta yenye thamani ya Tanzania Shiling 2,000,000/= kwa Katibu wa UVCCM  Wilaya ya Dimani Kichama, Nd. Ramadhan Abas Mcheju katika ghafla iliofanyika Tawi la CCM Kiembesamaki (Picha na Abdalla Omar).
Mjumbe wa NEC Chama cha Mapinduzi Amina (Mama Afrika) akimkabidhi Fedha Tanzania Shiling Laki 500,000/= Katibu wa UVCCM Jimbo la Kiembesamaki Zainab Idrissa Shani katika ghafla iliofanyika Tawi la CCM Kiembesamaki (Picha na Abdalla Omar).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.