Habari za Punde

Wanawake Shehia ya Tumbatu watakiwa kujitokeza kutoa tarifa za utelekezwaji

Sheha wa shehiya ya tumbatu jongowe Miza Ali Sharif.


Na Mwajuma Juma

SHEHA wa Shehiya ya Tumbatu Jongowe, Miza Ali Sharif amesema kuwa wanawake  wa eneo lake wamekuwa kimya kutoa taarifa za utelekelezwaji kwa kuhofia kunyooshewa vidole ‘Kutengwa’.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika shehiya hiyo alisema kuwa katika shehiya yake kumekuwepo na vitendo vya utekelezaji wanawake na watoto walioachika lakini wanashindwa kutoa ripoti.

Alisema kuwa mpaka sasa tokea kutumikia nafasi hiyo amepokea lalamiko moja tu la mama ambae ameachwa na mumewe na baadae kuachiwa watoto pasipo na kusaidiwa.

“Si kama matendo haya hayapo lakini wanawake wenyewe wanashindwa kutoa taarifa kwa kuhofia kuonnyeshewa vidole”, alisema Sheha huyo.

Hata hivyo akizungumzia kuhusu utelekezaji wa wanawake kwa wanaume wanaoenda dago kuvua alisema kuwa hilo limepunguwa kwa kiasi kikubwa kutokana na wanaume sasa kuwekea muda maalumu wa kukaa dago.

Alisema kuwa hilo wamefanikiwa kuliweza kutokana na kuunda kanuni ndogo ndogo ambazo zinawapa muda maalumu wa kukaa huko pamoja na kuwalazimisha kutoa matunzo kila mwezi kwa kila kipindi wanachokaa.

Hivyo aliwataka wanawake kutokaa kimya na badala yake wajitokeze kutoa ripoti kwa matendo yote ambayo wanafanyiwa ikiwemo kutelekezwa na watoto.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.