Habari za Punde

FUVU LA KICHWA CHA MWANAFUNZI ALIYEUAWA SCOLASTICA LILIVUNJIKA-SHAHID

Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi ambako shughuli za mahakama kuu kanda ya Moshi zimefanyika katika usikilizaji wa shauri la Mauaji ya Mwanafunzi wa kidato cha Pili katika shule ya sekondari ya Scolastica mjini Moshi.
Baadhi ya ndugu wa Washatwakiwa wakiwa katika chumba cha mahakama.
Washtakiwa katika shtaka la Mauaji ya Mwananfunzi wa Shule ya Sekondari ya Scolastica ,Humphrey MAkundi ,aliyebeba chupa ya maji ni Hamisi Chacha ,Laban Nabiswa (mwenye shati nyeupe)  na Edward Shayo wakisindikizwa na askari kuingia katika chumba cha Mahakam kwa ajili ya usikilizwaji wa shauri linalowakabili,
Mshitakiwa wa pili katika shtaka la mauaji ya Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Scolastica ,Edward Shayo akiingia katika chuma cha Mahakama wakati shtaka linalomkabili yeye na wenzake lilipoanza kusikilizwa .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.


SHAHIDI wa kwanza katika shauri la mauaji ya kukusudia namba (CC  48/2018) ,Dkt Alex Mremi ameieleza Mahakama kuu Kanda ya Moshi kuwa  wakati wa uchunguzi wa mwili wa Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Scolastika  Humphrey Makundi walibaini uwepo wa jeraha kubwa katika paji la uso na alivunjika fuvu la kichwa.


Mbele ya  Jaji  mfawidhi  wa mahakama kuu ,Divisheni  ya rushwa  na uhujumu Uchumi Dar es salaam ,Firmin Matogolo ,shahidi huyo ambaye ni Daktari Bingwa na Mkuu wa kitengo cha Patholojia alieleza kuwa  katika uchunguzi  huo pia walibaini jeraha kubwa lililokuwa kwenye paji la uso lilisababishwa na kupigwa na kitu kizito kisicho na ncha.


Akiongozwa na  Wakili Mkuu wa serikali,Joseph Pande  anayewakilisha upande wa Jamhuri  ,Dkt Mremi ambaye ni Daktari Bingwa na mkuu wa kitengo cha Patholojia ,Hoapstali ya Rufaa ya KCMC alieleza kuwa ukubwa wa jeraha lilolkuwa katika Paji la uso lilikuwa na ukubwa wa sentimita 6 kwa 5.


“Katika uchunguzi tulibini mwili wa marehemu ulikuwa na Nguo,T shirt ,Bukta pamoja na sox na lengo la uchunguzi huu lilikuwa ni kubaini chanzo cha kifo cha marehemu na tulibaini ni uwepo wa jeraha kiasi cha kuvunja mfupa,kitaalamu ni jeraha hilo ndio lilisababisha umauti”alieleza Dkt Mremi.


Dkt Mremi ambaye pia ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Tumaini  aliieleza mahakama kuwa mwili waliyofanyia uchunguzi ulikuwa ni wa mtoto mwenye umri kati ya miaka 15 na 17 huku akieleza sababu zilizopelekea kutambua hilo ni kutokana na muonekano wa meno.


“Meno yanaota kulingana na umri ,tulichobaini marehemu meno ya mwisho “Magego” yalikuwa bado yako chini hayajaota na alikuwa na majeraha mengine yalikuwa mabegani,Mgongoni na mapajani haya hayakuwa makubwa ukilinganisha na lile la kwenye paji lauso”alieleza Dkt Mremi.


Alieleza kuwa yapo maswali waliyojiuliza moja wapo ni kuwa marehemu alihusiana na nani,ndipo wakachukua sampuli katika maeneo ya mwili wa marehemu ili kubaini vinasaba (DNA) huku akitaja maeneo hayo kuwa ni mifupa kwenye mapaja,Mbavu na nyama kutoka sehemu za siri na kwenye makalio.


Akieleza sababu za kuchukua sampuli katika maeneo mbalmbali ya mwili ,Dkt Mremi alieleza kuwa kutokana na mwili kuanza kuharibika walilazimika kuchukua maeneo hayo ili kurahisisha usomaji wa vinasaba(DNA).


“Kwenye Jeraha tulichukua kipnde cha mfupa n nyama nyama kwenye maeneo yenye mchubuko ili kupata tissue zitakazo saidia kuangalia kwa ukaribu kitaalamu tunaita Histopathology ,kutizama kwa undani zaidi ya macho ya kawaida”alieleza Dkt Mremi.


Dkt Mremi alieleza kuwa uchunguzi huo husaidia kubaini jeraha lililokuwepo katika mwili wa marehemu huyo kama ni limekuwepo kabla ya kifo ama baada ya kifo na kwamba kilichoonekana majeraha hayo marehemu aliyapata wakati bado akiwa Hai.


“Tulichukua pia Sampuli ya meno na vipimo vya Damu kwa wazazi wa marehemu ,ambapo pia tulichukua sampuli ya ute wa mate na hizi tulichukua kwa mtu aliyetambulishwa kwentu kama baba wa marehemu ,aliyetambulishwa kwa jina la Jackson Makundi na mama Makundi.”alieleza Dkt Mremi.


Alieleza kuwa baada ya kukamilisha taratibu zote za kiuchunguzi walikabidhi mwili wa marehemu kwa ndugu na kisha kuandaa taarifa ambayo ilitiwa saini na madaktari wote walioshiriki katika uchunguzi huo uliofanyika katika chuma cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya KCMC.


Kuhusu kilichoandikwa katika ripoti hiyo Dkt Mremi alieleza kuwa kulikuwa na maelezo ya kile kilichobainika katika uchunguzi wao ikiwemo jeraha kubwa katika paji la uso linalotajwa kuwa sababu kubwa ya kifo pamoja na michubuko na kuiomba Mahakam kuipokea kama kielelezo katika shauri hilo.


Upande wa utetezi katik a shauri hilo linalovuta hisia za watu ,wakili David Shiratu ktika maswali kwa shahidi alitka kujua kwa nini katika uchunguzi huo hawakutumia kifaa maalumu cha Carbon 14 ili kujua umri sahihi wa marehemu .


“Mlikadiria umri wa marehmu ni kati ya miak 15 na 17 ,ni kwa nini hamkutaka kutumia Carbon 14 ili kujua umri wa mwili mliokuwa mnauchunguza”aliuliza Shiratu .


Akijibu swali hilo Dkt Mremi alieleza mahaka kuwa zipo njia nyingi za kubaini umri na njia waliyotumia ilikuwa ni mojawapo  huku akileza kuwa matumizi ya Carbon 14 yangeongeza gharama na kwamba hawakuhitaji njia ngumu kupata Vinasaba.


Shauri la mauaji  ya mwanafunzi  Humphrey Makundi aliyekuwa akisoma kiato cha pili katika  sekondari ya Scolastika imeanza kusikilizwa mfululuzo  likimkabili mmiliki wa shule hiyo ,Edward Shayo,Mwalimu wa nidhamu Labani  Nabiswa  na mlinzi wa shule ,Hamis Chacha.


Wakati wa usikilizwaji wa awali Agosti 27 2018 mbele  ya jaji Haruna Songoro ,upande wa mashtaka  ukiongozwa  wakili wa serikali mkuu Joseph  Pande,ulieleza utaita  mashahidi 34 katika kesi hiyo.


Pia,Pande aliijulisha mahakama kuwa  kuwasilisha vieelelezo vya nyaraka 15 yakiwamo maelezo ya kukiri kosa ya mshtakiwa  Chacha  akiwa polisi na kwa mlinzi wa amani.


Mbali na nyaraka hizo ,watawasilisha taarifa  ya mawasiliano  ya simu kutoka kampuni ya Vodacom inayodaiwa kuonyesha  washtakiwa waliwasiliana muda na siku ya mauaji.


Mbali na vielelezo hivyo ,upande  huo wa mashtaka  ulieleza mahakama   kiuwa utawasilisha vielelezo halisi (physical or real) ambavyo ni simu saba ,panga moja na nguo za marehemu.


Kwa upande wa mawakili wa utetezi,wao waliiambia Mahakama  kuwa orodha ya mashahidi wao  pamoja na vielelezo  watakavyotumia ,wataviwasilisha kabla ya washtakiwa kuanza kujitetea.


Mwanafunzi huyo alitoweka shuleni mnamo Novemba 6,2017 na baadaye kubainika ameuawa  na watu wasiojulikana baada ya maiti ya mtu aliedaiwa ni mtu mzima mwenye  ndevu ,kufukuliwa kwa amri ya mahakama.


Mwili wa mtoto huyo uliokotwqa Novemba 10,2017 katika mto Ghona mita 300 kutoka  shuleni hapo ,polisi waliuchukua  waliupeleka Hospitali ya Mawenzi na kuzikwa kwa madai haukutambuliwa .kwakuwa mwili huo ulishaanza kuoza na ulikuwa haujatambuliwa ,ulizikwa siku iliyofuata  ya Novemba 11 na Manispaa ya Moshi  katika makaburi ya kranga  yaliopo mjini hapa.


 Upande wa Jamhuri katika Shauri hilo unawakilishwa na Wakili wa serikali Mkuu ,Joseph Pande,Wakili wa serikali Mwandamizi ,Abdala Chavula,Wakili wa serikali Mwandamizi ,Omary Kibwana  na Wakili wa serikali Lucy Kiusa.


Upande wa utetezi unawakilishwa na Wakili wa kujitegemea Elikunda Kipoko na Gwakisa Sambo wanaomtetea  mshtakiwa wa pili ,Wakili wa kijitegemea David Shilatu anayemtetea mshitakiwa wa kwanza na Patrick Paul anaye mtetea mshtakiwa wa tatu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.