Habari za Punde

Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Yatembelea Miradi Kisiwani Pemba


MWENYEKITI wa kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya baraza la Wawakilishi Zanzibar, Hamza Hassan Juma akizungumza katika kikao cha kupokea taarifa ya robo ya tatu ya Januari-Machi kwa wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, huko mjini Chake Chake
BAADHI ya Wakurugenzi na watendaji wengine wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji  Zanzibar, wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa robo ya tatau ya wizara hiyo, kwa wajumbe wa kamati ya Ardhi na Mawasiliano kikao kilichofanyika mjini Chake Chake
KATIBU Mkuu izara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe, akisoma taarifa ya Robo ya Tatu ya Wizara hiyo kwa wajumbe wa kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya baraza la Wawakilishi Zanzibar, kikao kilichofanyika mjini Chake Chake
WAJUMBE wa kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakipitia baadhi ya vipengele katika taarifa ya robo ya tatau ya Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, kikao kilichofanyika Mjini Chake Chake
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.