Habari za Punde

Shamrashamra za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Songwe Tanzania.

 Vijana wa Halaiki wakionesha picha ya Mwl. Julius K. Nyerere wakati wakiimba nyimbo ya kumsifu kwenye hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu akiwa pamoja na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakifuatilia matukio ya vijana halaiki. (Kulia) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Kushoto) ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Balozi Ali Karume.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu akihutubia wananchi wa Songwe walioshiriki kwa wingi katika uwanja wa Kimondo – Forest, Wilayani Mbozi kushuhudia uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa Mwaka 2019.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Mkoa wa Songwe waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Songwe walioshiriki kwenye hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2019.
Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Balozi Ali Karume akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye Uwanja wa Kimondo, Wilayani Mbozi
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela akieleza jambo kuhusu Mkoa wa Songwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu akiwasha Mwenge wa Uhuru kuashiria uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa Mwaka 2019, Mkoani Songwe.
Sehemu ya Vijana wenye dhamana ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 (waliosimama mstari wa mbele).
Baadhi ya wananchi wa songwe wakifuatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu (hayupo pichani). Makamu wa Rais alikuwa Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2019. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.