Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein Awasili Kisiwani Pembe Leo Kwa Ajili ya Ufunguzi wa Majengo Pacha ya Wizara Tatu Kesho.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Hemed Suleiman alipowasili Uwanja wa Ndege wa Chakechake Kisiwani Pemba, kuhudhuria hafla ya Ufunguzi wa Majengo ya Kisasa kwa Ajili ya Wizara Tatu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Kisiwani Pemba yaliojengwa katika eneo la Gombani.kushoto Mshauri wa Rais Kisiwani Pemba Mhe. Maua Daftari. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mshauri wa Rais Pemba Mhe.Dkt Maua Daftari alipowasili Uwanja wa Ndege wa Chakechake Pemba jioni leo kuhudhuria Ufunguzi wa Majengo Pacha ya Wizara Tatu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kesho.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akielekea chumba cha mapumziko baada ya kuwasili Kisiwani Pemba kuhudhuria Ufunguzi wa Majengo Pacha ya Wizara Tatu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zilizongenjwa katika eneo la Gombani Pemba.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.