Habari za Punde

Mke wa Rais wa Tanzania Mama Janeth Magufuli AToa Futari Kwa Ajili ya Familia Zenye Mazingira Magumu Jijini Dar es Salaam

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi mmoja wa wawakilishi msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam jana Jumatano Mei 22, 2019(Picha na Ikulu)
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mama Janeth Magufuli, akiongea machache wakati wa hafla ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mama Janeth Magufuli, akimsiliza Katibu Mkuuwa BAKWATA Sheikh.Nuhu Muma akitoa shukurani wakati wa kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam 
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi Katibu Mkuu wa BAKWATA Sheikh.Nuhu Muma msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi Mkurugenzi wa Hija wa BAKWATA Sheikh Haidary Kambwile msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhita jijijini Dar es salaam

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwa katika  picha ya kumbukumbu na Katibu Mkuu wa BAKWATA Sheikh. Nuhu Mruma, Mkurugenzi wa Hijja wa BAKWATA Sheikh.Haidary Kambwile pamoja na wawakilishi wa vikundi mbalimbali vya wenye uhitaji baada ya hafla ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji.


Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama  Janeth Magufuli, amewasihi Waislamu nchini kuendelea kuliombea Taifa muda wote, hususan katika kipindi hiki cha  Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, na kuendeleza mshikamano bila kujali dini ama kabila tabaka zao.

Mama Magufuli ametoa wito huo leo tarehe 22 Mei, 2019 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji.

Vyakula alivyotoa ni tani 5 za mchele, tani 3 za sukari na tende. Hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa BAKWATA Sheikh Nuhu Mruma, Mkurugenzi wa Hijja wa BAKWATA Sheikh.Haidary Kambwile na wawakilishi wa vikundi mbalimbali vya wenye uhitaji.

Mama Magufuli pia amemuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema, azikubali funga za Waislamu wote na kuwalipa malipo stahiki wakati wa kitekeleza moja ya nguzo muhimu za Dini ya Kiislamu.

“Kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni kipindi cha toba. Ni kipindi cha kutenda matendo mema na kujizuia na vitendo viovu” amesema Mama Magufuli.

Mama Magufuli amesema licha ya kwamba Tanzania ina watu waimani za Dini tofauti lakini siku zote wananchi wake wamekuwa wakishirikiana nyakati za dhiki na za raha bila ubaguzi.

Ametoa mfano kuwa licha ya tofauti za kidini zipo baadhi ya familia ambazo Baba Muislamu na Mama ni Mkristo zinaishi kwa amani na kushirikiana katika masuala yote ya kifamilia na kwamba sifa hii ni moja nguzo muhimu za umoja wa Watanzania.
“Binafsi na kumbuka zamani nikiwa mdogo tulikuwa tunatafuta Mwislamu aje atuchinjie kuku ama mbuzi ama ng’ombe” ,alisema na kuongezea:

 “Ni kutokana na utamaduni huo uliojengeka miongoni mwa Watanzania , leo nimeguswa kutoa sadaka yangu kwa ajili ya ndugu zangu wenye uhitaji…”

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.