Habari za Punde

TIF UAE AID Wagawa Msaada wa Futari Kwa Wananchi wa Lindi.


Na,Mrisho Salum.
TAASISI ya The Islamic Foundation kwa kushirikiana Umoja wa nchi za falme za kiarabu UAE wametoa msaada wa vyakula wa tani 7 kwa watu Zaidi ya 100 wasiojiweza kuanzia wazee, wajane, watu wenye ulemavu pamoja na watu wenye uhitaji.

Msaada huo umetolewa katika Kijiji cha Moka Wilaya ya  Lindi Vijijini Mkoani Lindi ambapo msaada huo umezinufaisha Kaya 100 ambapo mahitaji hayo ya chakula ni mchele kg20, unga wa sembe kg20, maharage kg 10 , sukari kg 5 pamoja na mafuta ya kupikia lita 3 chakula ambacho kitawatosheleza kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi wa Idara ya Daawa wa Taasisi ya The Islamic Foundation Sheikh Ismail Rajab Kundya amesema kuwa taasisi ya the Islamic foundation imekuwa ni daraja  muhimu lakupitishia msaada huo kutoka umoja wa nchi za falme za kiarabu UAE kwenda kwa walengwa.

Aidha amesema kuwa Taasisi ya the Islamic foundation imekuwa ikiaminiwa na wahisani kwa kuwa imekuwa ikitekeleza miradi kwa uwazi na ukweli na kwamba mwenyekiti wake Aref Nahdi amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha misaada inawafika kwa wakati wenye uhitaji katika mikoa mbalimbali ya nchi ya Tanzania.

Amesema mwaka huu wanatekeleza mradi wa ufutirishaji kwa wafungaji ambapo lengo la mradi huo kuakikisha kaya ya watu sita wanapata futari inayokidhi kwa muda wa mwezi mzima na kusisitiza kuwa,Mradi huo unatekelezawa na taasisi ya the islamic foundation kupitia ushirikiano wa karibu na wahisani wa UAE AID kutoka umoja wa falme za kiarabu. 

Huo ni muendelezo wa ugawaji wa misaada mbalimbali kwa wahitaji zoezi ambalo limekuwa likitekelezwa na taasisi ya The Islamic Foundation mara kwa mara kupitia wahisani wa ndani na nje ya nchi ambapo mara hii imefanikiwa kugawa kikapu hicho cha chakula kwa ajili ya matumizi ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani.

Mpaka sasa Taasisi ya the islamic Foundation kwa kushirikiana na umoja wa falme za kiarabu UAE  wameweza kutoa msaada wa Iftari kwa mikoa ya Morogoro ambapo watu zaidi ya 1000 wenye mahitaji wamenufaika huku katika jiji la dar s salaam maimamu zaidi ya 750 wamenufaika na mradi huo wa ufuturishaji na mkoa wa lindi katika kijiji cha moka zaidi ya watu 100 wamenufaika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.