Mkurugenzi Mtendaji
wa MOI Dkt Respicious Boniface akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la
kimataifa la madaktari bingwa wa mifupa linalofanyika Tanzania (MOI) Kuanzia
tarehe 26 -30 May 2019 katika ukumbi mpya wa mikutano MOI
Madaktari wa Mifupa
kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia mada katika kongamano la kimataifa
linalofanyika MOI
Madaktari wa Mifupa kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia mada katika kongamano la kimataifa linalofanyika MOI
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dkt Respicious Boniface leo amefungua
kongamano la kimataifa la madaktari wa Mifupa linalofanyika kwa siku tano hapa
Tanzania ambapo madaktari zaidi ya 150 kutoka mataifa ya Afrika na sehemu
mbalimbali duniani wanashiriki.
Dkt Boniface amesema Kongamano hilo
limekua likifanyika hapa nchini kila mwaka kwa lengo la kuwajengea uwezo na
kuwapa mbinu mpya za matibabu ya mifupa madaktari hapa nchini na nchi nyingine
barani Afrika kutokana na MOI kuwa kituo cha mafunzo kutokana na huduma bora za
mifupa inazotozitoa.
“Madaktari bingwa wetu hapa nchini
wamekua wakinufaika sana na kongamano hili, wamekua wakipewa mbinu mpya na
zakisasa za matibabu na upasuaji wa mifupa jambo ambalo limepelekea MOI kuweza
kumaliza rufaa za nje ya nchi kwa wagonjwa wa mifupa ambapo kwa sasa huduma
karibia zote zinapatikana hapa nchini” Alisema Dkt Boniface.
Mratibu wa Kongamano hilo Dkt Joseph
Mwanga amesema mafunzo yatatolewa kwa njia ya nadharia, vitendo katika chumba
cha maabara kwa kutumia mifupa bandia na kwenda kwenye chumba maalum cha
kujifunzia kwa kutumia miili ya binadamu (Cadavers).
“Kongamano hili limekua na manufaa
makubwa sana kwetu, tumekuwa tukipata mbinu mpya kila mwaka kutoka kwa wenzetu
wa Marekani jambo ambalo limefanya huduma za mifupa hapa nchini ziendelee kuwa
bora ukilinganisha na mataifa mengine barani Afrika” Alisema Dkt Mwanga.
Kwa upande wake Profesa Michael Terry
ambaye ni mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Calfonia cha San Francisco amesema
ushirikiano kati ya Taasisi yake na MOI umejikita katika mafunzo ya namna ya
kuwahudumia majeruhi wa ajali kwa lengo la kuwapa huduma bora na za kisasa kwa
wakati.
Kongamano hilo limeratibiwa na
Taasisi ya MOI kwa kushirikiana na Taasisi za IGOT, SIGN, OTA, AO Alliance na
Chuo kikuu cha Calfonia San Fransisco Marekani.
Imetolewa na
Kitengo cha
Uhusiano MOI
No comments:
Post a Comment