Habari za Punde

Mvua za Masika Zinazoendelea Kunyesha Sehemu Mbalimbali Kisiwani Pemba Zaleta Uharibifi Katika Miundombinu ya Barabara.

KAZI ya ufukiaji wa kifusi katika eneo la barabara ya Kifumbi kai lililomegwa na maji ya mvua, ikiwa ineendelea kufanywa na mafundi wa Idara ya UUB Pemba, ambapo idara hiyo inatarajia kutumia milioni 30 kwa kazi ya ujenzi wa kuta tatu za mawe na baraza ya zege, kama ilivyofanya eneo la Kizimbani ili maji hayo kumwagika bila ya kuleta athari nyengine.
BAADHI ya mawe ambayo tayari yameshawekwa kwenye eneo lililoporomoka la barabara ya Kifumbi Kai, kwa ajili ya ujezi wa kuta tatau kubwa na baraza ya zege, kwa lengo la kuyafanya maji kumwagika bila kusababisha athari nyengine katika eneo hilo.
AFISA Mdhamini Wizara ya Ujenzi Mawasiliani na Usafirishaji Pemba, Hamad Ahmed Baucha akitoa maelezo kwa viongozi wa kamati ya sisasa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati walipotembelea eneo la barabara ya kifumbi kai iliyo haribika na mvua, mwenye kanzu mwenyekiti wa kamati hiyo Mberwa Hamad Mberwa katikati ni mwenyekiti wa mfuko wa barabara Mwajili Haji Mwajili
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.