Habari za Punde

KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balaozi Joseph Sokoine akiongea na Waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akitoa maelezo kuhusiana na zoezi zima la katazo la mifuko ya plastiki. Pembeni yake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Kanizio Manyika.


Mtakumbukakuwa 9 Aprili 2019 SerikaliilitoaTamko la kusitisha matumizi ya Mifuko ya 
plastiki hapa nchini ifikapo Juni Mosi 2019. Katazo hili linalenga kuepusha athari za kiafya na mazingira zinazoendelea kujitokeza kutokana na matumizi ya mifuko hiyo.

Katazo hilo lililotolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kasssim Majaliwa linahusu kupiga marufuku uzalishaji, uingizaji, usafirishaji nje ya nchi, usambazaji, uuzaji na matumizi ya mifuko ya plastiki ya aina zote.

NduguWanahabari:
Ofisi ya Makamu wa Rais imekuwa ikitoa taarifa mbali mbali ili kuwaelimisha wananchi kuhusu katazo hilo kupitia Vyombo vya Habari ikiwa ni pamoja na magazeti, Runinga na Redio, Mitandao ya Kijamii, Mikutano ya wadau na kupitia mikusanyiko ya watu ikiwa ni pamoja na taarifa kusomwa katika nyumba za ibaada.

Mpaka sasa Serikali imetekeleza yafuatayo:
1.
Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa Kanuni kuhusu Katazo hili. Kanuni hizi zitaanza kutumika tarehe 1 Juni 2019. 
Kwa mujibu wa Kanuni hizi, itakuwa ni marufuku kuzalisha, kuingiza nchini, kusambaza na kutumia mifuko ya  plastiki iliyotajwa katika Katazo hili. Kiwanda, Kikundi cha Watu 
au  Mtu Binafsi atakayebainika kukiuka matakwa ya  Kanuni hizi atakuwa ametendakosa la  ji naina hivyo sheria itachukua mkondo wake.

2.     Tumetoa maelekezo Mahsusi kwa Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji  wa katazo hili ambapo baadhi yao wameanza kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya uhifadhi wa shehena ya mifuko itakayosalimishwa
 3.     Kwa kushirikiana na Makampuni ya Simu ya Vodacom, Tigo, Airtel na Halotel tumefanikiwa kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu kwa watumiaji wa mitandao hiyo ambapo watumiaji milioni  11 wa Tigo, Milioni 15.5 wa Vodacom wameshapata ujumbe huu, hii itakuwa endelevu kila wiki 4.     
Tumeandaa  na kusambaza taarifa kwenye taasisi za dini ili nao watusaidie kufikisha ujumbe huu kwa waumini wao, tunawashukuru sana wameitikia witov izuri.

5.     Tumekutana na wazalishaji wa mifuko mbadala wa plasti kina wamepanga kuongeza kasi zaidi uzalishaji wa bidhaa hii na baadhi wameshaagiza mitambo ya kuzalisha mifuko mbadala.

6.     Tunaendelea kutoa matangazo kwa kutumia vipaza sauti katika ngazi ya Kata, Mitaa na Vijiji kila wiki 7.     Tumeendelea kutoa elimu kupitia Vyombo vya Habari ikiwa ni pamoja na kufanya Media Tour, kutoa ‘Count down’ kwenye magazeti, kutumia redio za kijamii na redio za mikoani kutoa matangazo juu ya katazo hili.

 Pia tumetumia mitandao ya kijamii (Tovuti, blogs, facebook, twitter na istagram) bila kusahau katuni ili kuhakikisha ujumbe unafika kote.

8.     Tumetengeneza Bronchure, fliers, Banners na stickers na tunahakikisha tunawasambazia watu wote ili wapate uelewa ikiwa ni pamoja na wasafiri katika Vyombo vya usafiri
9.     Tunaendelea na utoaji wa Makala maalumu katika magazeti na kutumia redio kurusha matangazo yetu.

NduguWanahabari:
Jitihadazotehizizinapaswakuungwamkononasikubezwa, pianitoeraikwawatanzaniawotekutopotoshajambohilikamailivyofanywajuzikatikakipande cha video(Clip)iliyosambazwakatikamitandao ya kijamii. Na kipandehikoni cha mwakajana 2018 wakati wa kikaokilichoandaliwanaOfisi ya Makamu wa RaiskuzungumzanaWadau wa mifuko.
Ikumbukwekuwaifikapotarehe1 Juni 2019, Serikaliitaendeshaopereshenikabambenchinzima ya kusakamifukohii.OpereshenihiiitahusishaVyombovyaUlinzinaUsalama, KamatizaUlinzinaUsalamazaMikoanaWilaya, MamlakazaSerikalizaMitaaMamlaka ya Maabara ya MkemiaMkuu wa Serikali, Shirika la Viwango la Taifa (TBS), Mamlaka ya ChakulanaDawa (TFDA), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, pamojanaMamlakazaViwanjavyaNdege, Bandari, Forodha, Uhamiaji, naUsafiri wa NchiKavu.
Kwa wale ambaowatakuwatayarikusalimishakwahiarishehena ya mifukowatakayokuwanayo, utaratibuutatolewa wa mahalirasmiwanapotakiwakuisalimishakwenyemaeneoyao.
Kwataarifazaidikuhusuutekelezaji wa katazohiliWananchikwaujumlamnashauriwakutembeleaOfisiza Kanda zaBaraza la Taifa la HifadhinaUsimamizi wa Mazingira (NEMC) zilizopo Dar es Salaam, Mtwara, Dodoma, Mbeya, Mwanza, KigomanaArusha. Aidha, wanawezapiakuwasiliananaWakurugenzi wa HalmashaurizaMajiji, ManispaaMijinaWilaya.

Nirudie tena kutoa taarifa kwa Watanzania wote kuzingatia maelekezo haya ya Serikali pamoja na matakwa ya Kanuni za kupiga marufuku matumizi na biashara ya mifuko ya plastiki nchini kwa mustakabali wa uhifadhi wa mazingira ya nchi yetu.
Asantenikwakunisikiliza,

Imetolewana:

BaloziJoseph E. Sokoine
NAIBU KATIBU MKUU, OFISI YA MAKAMU WA RAIS
11 MEI, 2019

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.