Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Ndugu Fatma Hamad Rajab akishirikiana na Kamati ya Maandalizi ya Msimu wa tatu wa mbio za Stop GBV Half Marathon wakizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo , Migombani,Wilaya ya Mjini .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Ndugu Fatma Hamad Rajab amesema ifikapo Novemba 30, 2025,kutafanyika msimu wa tatu wa mbio za Stop GBV Half Marathon katika mji Mkongwe Zanzibar kuanzia saa 11:30 asubuhi na kuwashajihisha wananchi kuunga mkono mashindano hayo.
Akitoa taarifa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali akishirikiana na Kamati ya Maandalizi ya Mbio hizo katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Migombani.
Amesema lengo kuu la mbio za mwaka huu ni kurejesha matumaini kwa mama aliyeathirika na vitendo vya ukatili wa kijinsia hususan wale waliotelekezwa na wenzi wao baada ya kujifungua pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu.
Aidha amesema kupitia mbio hizi jamii inahamasishwa kujenga moyo wa huruma mshikamano, uwajibikaji katika malezi na ustawi wa familia.
Nae Kiongozi wa maandalizi hayo Asma Mwinyi Foundation amesema kunatarajiwa kwa mwaka huu kuwa na washiriki kutoka mataifa mbali mbali kuja kushiriki katika mbio za umbali wa 5km, 10km na km 21 ambazo zimejipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya Zanzibar.
Amefahamisha kuwa mashindano hayo hufanyika ndani ya siku 16 za kupinga udhalilishaji wa kijinsia duniani sambamba na kutangaza kisiwa cha Zanzibar kuelekea kilele cha Mji Mkongwe tarehe 02 Disemba.
Ameelezea washiriki wa mbio za Stop GBV Half Marathon watapata zawadi za ushindi kwa wanaume na wanawake kwa mbio za km21kwa mshindi wa mwanzo milioni sita na watano milioni moja .kwa km 10, Mshindi wa mwanzo shilingi milioni moja na laki tano na wa tano ni laki tano pamoja na washindi wa sita wa mwisho kujinyakulia laki moja.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa Uhifadhi wa Mji Mkongwe Ali Bakar amesema amekuwa na mashirikiano ya karibu katika kuendeleza Tamasha hilo ambalo linatarajiwa kufanyika katika kuelekea kilele cha kuanzimisha siku ya mji mkongwe kila ifikapo 2, Disemba siku ambayo uliasisiwa na kupewa hadhi ya Urithi wa dunia.
Amesema tamasha hilo la msimu wa tatu licha ya kupinga vitendo vya ukatili na udhalilishaji pia itakuwa ni fursa ya kuutangaza mji mkongwe kiutalii sambamba na wafanya biashara wadogo wadogo wa aina mbali mbali kuweza kufanya bishara zao.
Msimu wa tatu wa mbio za Stop GBV Half Marathon. zinatambulika kimataifa na zinaorodheshwa katika kalenda ya riadha ya dunia (World Athletics Calendar ) ambazo zimeendele kuwa jukwaa muhimu ya kuhamasisha jamii kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia (GBV) sambamba na kuziunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutokomeza udhalilishaji katika Nyanja zote za maisha
Maelezo ya Picha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Ndugu Fatma Hamad Rajab akishirikiana na Kamati ya Maandalizi ya Msimu wa tatu wa mbio za Stop GBV Half Marathon wakizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo , Migombani,Wilaya ya Mjini .
Imetolewa na Kitengo cha Habari
WHVUM
No comments:
Post a Comment