Habari za Punde

United yamruhsu Pogba kuondoka

Kutoka.London, England.
KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, ameridhia na  kumruhusu Paul Pogba kuondoka wakati wa majira ya joto, ikiwa anaamua hataki tena kucheza katika timu hiyo.Mfaransa huyo anataka kuondoka klabuni hapo hasa baada ya United kushindwa kufuzu hatua ya kucheza ligi ya mabingwa Ulaya.United walimnunua kiungo huyo kwa kuvunja rikodi ya dunia kwa kutoka pauni milioni  89  mwaka wa 2016, na mwenyekiti mtendaji mkuu Ed Woodward anaona Pogba bado ni mtu muhimu klabuni hapo.
Woodward alimzuwia Pogba  kujiunga na Barcelona mwisho mwa majira ya joto wakati alipokuja kocha Jose Mourinho.Pogba ana miaka miwili iliyobaki kwenye mkataba wake huko Old Trafford.Hata hivyo inadaiwa kuwa Solskjaer na Woodward wanatofautiana  juu ya hatma ya baadaye ya Mfaransa huyo, na Solskjaer ameitaka klabu hiyo kuacha kumg’angania mchezaji ambaye hataki kuichezea timu.
Woodward anahisi Pogba anaweza kuharibu sifa ya United lakini Solskjaer anaweza kumchunga mchezaji huyo.Hata hivyo inasemekana kuwa Pogba ameamua kushinikiza kuondoka hata kama msimamo wa klabu ni kwamba hawataki kumuuza .
Wakala wake Mino Raiola, hakuwa tayari kuzungumza suala hilo hadi msimu huu utakapomalizika, na kuwaeleza kuwa mteja wake anataka kuondoka.United  inaweza kumuuza Pogba kwa  karibu pauni milioni   150.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.