Habari za Punde

Mvua za Masika Tayari Zimeshaaza Kuathiri Baadhi ya Makazi ya Wananchi

BAADHI ya wananchi ka􏰀ka shehia ya Mwanakwerekwe wakipigwa na mshangao kwa kuliangalia eneo ambalo mnara na tenki la kuhifadhia maji lilipodidia chini ya ardhi ka􏰀ka chuo cha Mwalim Waziri. Hali hiyo inatokana na athari ya mavua kubwa inayoendelea kunyesha. (PICHA NA ABDALLA MASANGU).
Na.Hafsa Golo Zanzibar.                                                                      KAYA 120 zilizomo ndani ya shehia tatu za jimbo la                 jangombe, zimepatiwa futari kutokana na kupata madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha.
Mwakilishi wa jimbo hilo, Ramadhan Hamza Chande, alieleza hayo wakati akizungumza na gazeti hili jimboni humo akiwa katika harakati za utekelezaji wa zoezi hilo.
Alisema ugawaji huo utafanywa sambamba na kaya nyengine 42 zilizomo katika shehia ya Mwembemadema ambayo ni jirani wa jimbo la Jang’ombe.
Alitaja  shehia tatu zilizomo ndani ya jimbo la Jang’ombe ni Jang’ombe Urusi, Jang’ombe na Kwaalinatu.
Alisema kaya hizo zitaendelea kuelimishwa juu ya umuhimu wa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na mamlaka ya hali ya hewa ili kunusuru uwezekano wa kutokea maafa.
Aliwaomba wananchi wa jimbo hilo na jamii kwa jumla  kuhakikisha wanafuata maelekezo ya wataalamu wa afya hasa katika kipindi hiki cha mvua ili kudhibiti maradhi ya mripuko.
Nae Sheha wa shehia ya Jang’ombe Urusi, Yusuf Juma Mtumwa, alisema, umoja na mshikamano na viongozi kuwahurumia wapiga kura wao ndio jambo la msingi pale wanapofikwa na maafa.
Mmoja wa wananchi ambae nyumba yake iliathiriwa na maji, Suleiman Ramadhani, alisema tukio hilo ni kudra zake Mwenyezi Mungu hasa ikizingatiwa ni zaidi ya miaka mitatu sasa wananchi wa eneo hilo wanaendelea kuishi salama.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.