WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Simu ya Maandishi:
“ZIMAMOTO KUU”
Simu Nambari: +255-22-2113537
Nukushi:
+255-22-2184569
Baruapepe:
fire.rescue@frf.go.tz
Tovuti:
www.frf.go.tz
|
Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji
S.L.P. 1509
DODOMA
21 Mei, 2019
|
TAARIFA KWA UMMA
ADA
YA MAFUNZO YA KINGA NA TAHADHARI DHIDI YA MAJANGA YA MOTO KWA SHULE ZA MSINGI
NA SEKONDARI
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
limeundwa na linatekeleza majukumu yake chini ya Sheria ya Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji namba 14 ya mwaka 2007 (Fire and Rescue Force Act No. 14 of 2007) na Kanuni zake za mwaka 2008.
Majukumu makubwa ya Jeshi hili ni kuokoa Maisha na Mali katika majanga mbalimbali.
Sambamba na majukumu hayo
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linafanya ukaguzi wa Kinga na Tahadhari dhidi ya
majanga ya moto, na kutoa ushauri wa aina na namna ya uwekaji wa vifaa vya
kinga na tahadhari. Ukaguzi huu unafanyika kwa mujibu wa sheria namba 14 ya
mwaka 2007 ikisomwa pamoja na Kanuni ya Vyeti ya Usalama wa moto ya Mwaka 2008
na marekebisho ya mwaka 2014 (Fire and Rescue Force Safety Inspections and
Certificates Regulations of 2008 GN.106 and its Amendment GN 63 of 2014.)
pamoja na Kanuni ya Tahadhari dhidi ya moto kwenye majengo ya mwaka 2015 (Fire
and Rescue Force Fire Safety Precaution in Building Regulations of 2015
GN 516.) Ukaguzi huu huambatana na tozo kwa mujibu wa sheria na kanuni.
Hivyo
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linapaswa kutoa elimu katika sehemu mbalimbali
kama vile viwanda, mahoteli, maduka, shule za msingi na sekondari, migodi,
vituo vya mafuta n.k. Watumishi wa taasisi husika wanapaswa kulipia gharama za
mafunzo (training fee) ambazo ni shilingi 20,000/= kwa kila mshiriki kama
ilivyoainishwa katika kanuni za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Mafunzo hayo ya
kinga na tahadhari ya majanga ya moto hutolewa bure kwa wanafunzi wa ngazi
zote.
Jeshi
linatoa rai kwa Wamiliki na Wakuu wa Shule za Kutwa na Bweni ambazo
hazijapatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto kuwasiliana
na Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa husika ili waweze kupatiwa
elimu hiyo.
Imetolewa na;
Kitengo cha Habari,
Mawasiliano, Uhusiano na Elimu kwa Umma
Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji- Makao Makuu.
No comments:
Post a Comment