Bwana Ramadhan Ali Foum {Rama Kimara} akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Hospitali ya Kijitonyama kumkagua Mkewe Bibi Lela Ngozi Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa aliyelazwa kupatiwa huduma za Afya.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimjulia hali Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Bibi Lela Ngozi aliyelazwa Hospitali ya Kijitonyama Dar es salaam akipatiwa huduma za Afya.
Daktari dhamana wa Hospitali ya Kijitonyama Dr.Nyamsogoro akimuelezea Balozi Seif maendeleo ya Afya ya Mgonjwa wao Bibi Lela Ngozi wanayempatia huduma za Matibabu Hospitalini hapo.
Bibi Lela Ngozi akielezea faraja anayoipata kutokana na huduma za matibabu yake wakati akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Picha na – OMPR – ZNZ
No comments:
Post a Comment