Habari za Punde

Balozi Seif Azungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Kimataiufa ya Mtandao wa Viwanda ya Nchini Misri

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akizungumza na Timu ya Waaalamu Watano wa Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa Mtandao wa Viwanda ya Nchini Misri {I E S}.
Mhandisi Ibrahim Qamar wa Timu ya Waaalamu Watano wa Tawi la Kampuni  ya Kimataifa ya Uhandisi wa Mtandao wa Viwanda ya Nchini Misri akimkabidhi Balozi Seif Kitabu cha Historia ya Kampuni yake.










Na.Othman Khamis OMPR.
Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa Mtandao wa Viwanda ya Nchini Misri {I E S} imejitolewa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utanuzi wa Ujenzi wa Gati ya Malindi ili iendelee kutoa huduma za uteremshaji na upakiaji wa Mizigo kwa uhakika.
Timu ya Waaalamu Watano wa Tawi la Kampuni hiyo inayojishughulisha na masuala ya Uhandisi wa Umeme liliopo Afrika Mashariki ikiongozwa na Mhandisi Ibrahim Qamar ilitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
Mhandisi Ibrahim Qamar alimueleza Balozi Seif  kwamba Uongozi wa Kampuni hiyo umeridhika na harakati za Uchumi na Biashara Zanzibar zinazohudumiwa na Bandari hiyo ambayo kwa sasa inahitaji kuongezewa nguvu za utanuzi ili itoe huduma zilizo bora zaidi.
Alisema Zanzibar ni kituo cha Biashara cha Kimataifa kinachoendelea kuyaunganisha Mataifa mengi yaliyomo ndani ya Ukanda wa Bahari ya Hindi kwa masuala ya Biashara kwa Karne kadhaa zilizopita ambacho kwa sasa kinastahiki kurejeshewa hadhi yake ya asili.
Mhandisi Ibrahim alimthibitishia Balozi Seif  kwamba kutokana na umuhimu mkubwa wa Bandari ya Malindi Zanzibar katika utoaji wa huduma zake Uongozi wa Kampuni yake umeshajitolea katika harakati za Utanuzi huo muda wowote kuanzia sasa endapo utapatiwa fursa hiyo adhimu.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema ni vyema ukaandaliwa utaratibu Maalum kwa Wahandisi wao kukutanishwa na Wataalamu Wazalendo ili kulifanyia kazi suala hilo muhimu.
Balozi Seif  alisema mkutano huo wa pamoja utawezesha kuangalia njia za kufanya utafiti utakaotoa jibu la nanma Bandari hiyo inavyoweza kushughulikiwa katika utanuzi wake.
Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa Mtandao wa Viwanda ya Nchini Misri       {IES} iliyoasisiwa Mnamo Mwaka 1938 imekuwa ikitoa huduma katika Mataifa mbali mbali Barani Afrika pamoja na Mashariki ya Kati ikishirikiana pia kwa kuingia ubia Miradi tofauti na Makampuni kadhaa Ulimwenguni.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa Viongozi wa Wafanyabiashara kutoka Jimbo la Shadong Nchini china ukiongozwa na Meya wa Manispaa ya Mji wa Jimbo hilo Bwana Zhaogang Wang.
Katika mazungumzo yao Balozi Seif alisema Zanzibar bado ina fursa nyingi za Uwekezaji akatolea mfano Sekta Viwanda, Utalii, Mawasiliano na Biashara lakini mtazao wa sasa ni kuona eneo la Uvuvi wa Bahari Kuu linapewa Msukumo kama ilivyopewa Sekta ya Utalii.
Alisema Zanzibar imezunguukwa na Bahari sehemu zote mazingira ambayo Wawekezaji wa Jimbo la Shadong wanaweza kuitumia fursa hiyo kwa masuala ya uwekezaji kwa vile Nchi hiyo tayari imeshapiga hatua kubwa katika kuimarisha Uvuvi wa Bahari Kuu.
Balozi Seif alimuahidi Meya huyo wa Manispaa ya Shadong kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar muda wote itakuwa tayari kuwaunga mkon Wawekezaji wa Jimbo hilo na China kwa Ujumla pale watakapoamua kuanzisha miradi yao ya Kiuchumi Visiwani Zanzibar.
Mapema Meya wa Manispa ya Jimbo la Shadong Bwana Zhaogang Wang alisema China imefanya mabadiliko katika Sekta zake za Uwekezaji kwa kuwaruhusu Wafanyabiara Binafsi kuzitumia fursa hizo katika Mataifa mbali mbali Duniani.
Bwana Wang alisema ipo miradi ambayo Wawekezaji wa Jimbo hilo wameshaipanga katika mfumo wa Ubia na Taasisi tofauti Duniani zikiwemo Nchi za Bara la Afrika katika sekta za Uvuvi wa Bahari kuu pamoja na Kilimo cha kisasa.
Kwa upande wake Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imeshatliana saini Mkataba wa Ushirikiano kati yake na Uongozi wa Jimbo hilo kaika miradi mbali mbali ya Maendeleo.
Balozi Amina alisema miongoni mwa maeneo yaliyoguswa katika mkataba huo ni pamoja na ushirikiano ya pamoja katika mbinu za utunzaji wa mazingira kwenye Mji wa Rosha Jimboni Shadong na ule wa Zanzibar.
Ushirikiano huo pia umegusa eneo la bidhaa zinazotokana na mazao ya baharini, lakini kilichopo kwa sasa ni maendeleo ya Utafiti ya kina wa Mradi huo kabla ya kuaza utekelezaji wake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.