Habari za Punde

Mbunge wa viti maalum CCM Mkoa wa Mjini atoa vifaa vya Mil 15

 BAADHI ya Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT  Mkoa wa Mjini wakisikiliza nasaha za mgeni rasmi katika Ufunguzi wa Kikao cha Baraza Kuu la UWT Mkoa wa Mjini, kilichofanyika katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja
 MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja Bi.Ghanima Sheha akifungua Kikao cha Baraza Kuu la Mkoa huo,huko katika Ukumbi wa Mkoa wa Mjini ulioopo Amani Unguja.
 MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis Shomari (kulia),akimkabidhi Viti 50 Katibu wa UWT Jimbo la Magomeni Ndugu Khadija Rajab Pazi (kushoto)
MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Shomari Khamis akimkabidhi Katibu wa UWT Wilaya ya Amani Ndugu Asha Mzee Kiti Kimoja na Meza Moja vya Ofisi.
                                        
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis Shomari,amekabidhi Vifaa mbali mbali vyenye Thamani ya Shilingi Milioni 15 kwa Majimbo yote ya UWT ndani ya Mkoa huo.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Viti 451,Meza Moja ya Ofisi na  Mashine  Moja u ya kutengenezea Chaki ikiwa ni sehemu ya kuunga Mkoa juhudi za Ujasiliamali za Akina Mama wa Mkoa huo.
Akizungumza katika Hafla ya kukabidhi Vifaa hivyo Mbunge huyo Mhe.Faharia amesema lengo la kutoa Vifaa hivyo ni kutekeleza Ilani ya CCM ya Mwaka 2015/2020.
Mhe.Faharia ameeleza kuwa Akina Mama wa UWT ndani ya Mkoa huo pamoja na majukumu ya kisiasa waliyokuwa nayo bado wanatakiwa kujiajiri wenyewe kupitia ujasiriamali hivyo vifaa vilivyotolewa vitawasaidia katika harakati hizo za kujiajiri wenyewe.
Pamoja na hayo alitoa Wito kwa Wanawake wa rika mbali mbali ndani ya Mkoa wa Mjini kushiriki kaiunga Mkoa CCM ili ishinde katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.
Katika hafla hiyo Wawakilishi wa Viti Maalum wa Mkoa huo ambao ni Mhe.Mgeni Hassan Juma aliahidi kutoa Mashine mbili za Photocopy kwa UWT Wilaya ya Amani na Mjini huku Mhe.Saada Ramadhan amekabidhi Mifuko Mitano ya Jipusamu kwa ajili ya kutengenezea chaki na kuahidi shilingi Milioni Moja kwa kila jimbo la UWT.
Wakizungumza kwa wakati tofauti Makatibu wa UWT wa Majimbo yote yaliyomo katika Mkoa huo, wameahidi Vifaa hivyo kuvitunza na kuhakikisha wanavitumia katika matumizi yaliyokusudiwa.
Awali akifungua Kikao cha Baraza Kuu la UWT Mkoa wa Mjini Mwenyekiti wa Mkoa huo Ndugu Ghanima Sheha,amesema Kikao hicho kitajadili masuala mbali mbali ya kiutendaji na kutoa maelekezo ya kiutendaji juu ya ufanikishaji wa majukumu mbali mbali ya UWT na CCM kwa ujumla.                    

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.