Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni atoa fedha taslimu kwa vikundi vya ujasiriamali katika jimbo lake.

Wilaya ya Mjini.       
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi amewataka Wajasiriamali wa Jimbo hilo kusimamia Miradi ya inayoanzishwa na Viongozi wao ili iweze kuwasaidia kuondokana na tatizo la ugumu ya Maisha.

Ameyasema hayo huko wakati alipokuwa akikabidhi fedha taslim kwa Vikundi vya Ujasiriamali vya Hakuna tabu,Fundi Mnyonge na Mapilau Vilivyomo katika jimbo hilo.

Amesme vikundi vya Ujasiriamali vina mchango mkubwa ndani ya jamii hivyo iwapo wataienzi na kuiendeleza Miradi hiyo kutaweza kuwaletea maendeleo katika maeneo yao.

Aidha amewataka Wajasiriamali hao kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kuweza kupata soko la uhakika la kuuza Bidhaa wanazozizalisha.

Hata hivyo amewataka wanaochukuwa Mikopo kurejesha kwa Wakati ili wengine waweze kukopa na kuepukana na Migogoro isiyokuwa ya lazima.

Kwa upande wake Diwani wa Wadi ya Magomeni Mohd Said Mohd amewasihi Wazazi wa eneo hilo kuwashajiisha Watoto wao kujiunga na vikundi hiyvo ili waondokane na kukaa Maskani bila kufanya kazi yoyote.

Nao Wajasiriamali hao wamempongeza Mwakilishi huyo kwa kuwapa Msaada huo kwani utaweza kuwasaidia kuzalisha Mitaji ya uhakika na kuahidi kuutumia katika shughuli za kimaendeleo kama walivyo kusudia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.