Habari za Punde

Kikosi cha Timu ya Chiba Yakubali Kipigo Michuano ya Kipwida Kwa Bao 3 -2.

Na.Mwanajuma Juma.
TIMU ya soka ya Chiba FC imeshindwa kutamba mbele ya Mbao FC kwa kukubali kifungo Cha mabao 3-2 katika mchezo wa michuano ya kipwida yanayoendelea Mjini hapa.

Mchezo huo uliochezwa uwanja wa Maungani ulionesha kuwa na upinzani mkali kutokana na Kila mmoja kuwa na umuhimu mkubwa ili kuweza kujiweka katika mazingira mazuri.

Matokeo hayo yanaifanya timu hiyo kuongeza kundi A ikiwa na pointi nane wakati Chiba FC inakuwa wa pili ikiwa na pointi nne.

Katika mchezo huo Mbao mabao yake mawili yalifungwa na Zola Abdalla na moja likafungwa na Suleiman Ali wakati Chiba yakafungwa na Gulamu na Hassan Mbwele.

Kesho michuano hiyo inatarajiwa kuendelea tena kwa kupigwa mchezo Kati ya Uzi FC na Njaa Kali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.