Habari za Punde

*Tanzania na Brazil Zina Maeneo Mengi ya Kuimarisha Uhusiano na Kuendeleza Maslahi ya Pamoja.*Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Tanzania wakiwa katika moja ya mikutano yao wakiwa katika ziara Nchini Brazil kuzungumzia Uwekezaji na ushirikiano wa nchini mbili hizi.

Brazilia.

Ujumbe wa Tanzania uliojumuisha wafanya biashara kutoka sekta binafsi, baadhi ya wakuu wa mashirika ya umma na Maofisa ya Biashara wamefanya ziara ya kibiashara nchini Brazil yenye lengo la kutafuta fursa  za kibiashara, uwekezaji na masoko  kwa bidhaa zinozalishwa Tanzania.
Ziara hiyo  ya siku kumi ambayo imebuniwa na sekta binafsi  kwa mashirikiano na ubalozi wa Brazil nchini Tanzania na kuratibiwa kwa pamoja na Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Brasilia.Ziara hiyo ya kibiashara ya siku kumi ( 10)ambayo imeandaliwa na sekta binafsi ya Tanzania kwa mashirikiano na Ubalozi wa Jamhuri ya brazili nchini  Tanzania na kuratibiwa  mashirikano na wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki na ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Brazilia umejumuisha washiriki kumi na mbili ( 12) kutoka wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki, ofisi ya ubalozi wa heshima wa Brazil nchiniTanzania, jumuiya ya wafanya biashara Tanzania kampuni ya Zest limited, Kampuni ya Alpha Afrika, kampuni ya  KC Land Development Plan, Kampuni la Pivotec Company Ltd pamoja na Shirika la biashara la Taifa la Zanzibar(ZSTC) na Mamlaka ya Uthibiti wa Matumini wa Maji na Nishati Zanzibar(ZURA)


Katika Ziara hiyo ujumbe wa Tanzania umeona na kufanya mazungumzo na Taasisi mbali mbali za Brazil zikiwemo  shirika kuu la uchimbaji mafuta  na gesi ya Brazil Petrobras, kampuni ya shughuli za idhibiti, viwango na uendelezaji  wa masoko ya mafuta na gesi (IBP), Wakala wa uwekezaji na Biashara  ya Brazil (APEX), Muungano wa Jumuiya ya Wenye viwanda ya Brazil(NCI) na Taasisi ya Uendelezaji wa Wazalishaji wadogo na Wakati (SEBRAE) Taasisi nyengine ambazo ujumbe wa Tanzania ulikutana na viongozi na kuwa na mazungumzo ya ushirikiano ni Bodi ya Utalii ya Brazil(Embratur), Wizara ya Kilimo, Sehemu ya udhibiti wa biashara za Mazao ya matunda na mifungo, Muungano wa Wenye viwanda wa São Paulo na Taasisi ya uendelezaji wa Teknolojia na ununifu ya São Paulo. Ujumbe ulipata nafasi ya kutembelea Miji ya Rio de Janeiro , Brasilia, na São Paulo pamoja na kufanya mazungumzo  na kaimu na Maofisa wa ubalozi wa Tanzania jijini Brasilia na kukutana na Baadhi ya Diaspora wa Tanzania mjini São Paulo.


Katika mazungumzo na shirika la uchimbaji wa mafuta na gesi la Petrobras na Kampuni ya uendelezaji wa masoko na Udhibiti wa mafuta na gesi (IBP) ilibainika pamoja na kwamba kampuni ya Petobras imesitisha shughuli zake za utafutaji wa mafuta nchini Tanzania, nchi hizi mbili zinaweza kushishikiana katika maeneo mbali  yakiwepo kujenga Uwezo, kuendeleza utafiti, masoko shughuli za udhibiti wa bidhaa na viwango, kutafuta masoko pamoja na kubadilishana uzoefu na wataalamu. katika kuhakikisha utekelezaji wa hayo panda mbili zimekubaliana kuandaa mkataba mashirikiano na kusainiwa baada ya kukaribisha taratibu zinazohitajika.


Kuhusu masuala ya biashara na uwekezaji imeonekana kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa bidhaa za Tanzania kama vile korosho, karafuu na mazao ya bahari kupata soko nchini Brazil. Pia kuna uwezekano mkubwa kwa Kwa Tanzania kununua sukari kutoka brazil. Ubalozi wa Jamhuri ya Tanzania Brasilia umeahidi kufuatilia upatikanaji wa masoko hayo . Brazil ni mzalishaji mkubwa wa sukari na mazao ya mifugo. Katika mazungumzo ya ushirikiano wa uwekezaji ya uwekezaji yaliyofanyika katika  Makao makuu wakala wa uwekezaji (APEX) mjini Brasília ilibainika kuwa Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza katika taratibu za kuvutia wawekezaji kutoka nje na kuendeleza wawekezaji wa ndani. Pia pande mbili zilikubaliana kushirikiana katika kuendeleza fursa za uwekezaji na kubadilishana Taarifa. Vile vile ilibainika kuwa kwa hivi sasa Hakuna taarifa za kutosha kuhusu fursa ya uwekezaji zilizo Tanzania kwa hivyo ilitolewa wito kwa ofisi za Ubalozi wa Tanzania brasilia, ubalozi wa Brazil nchini Tanzania, wakala wa uwekezaji wa Brazil , mamlaka za uwekezaji na Tanzania na jumuiya ya wafanya biashara na sekta binafsi Tanzania kufanya biashara kwa karibu sana kwa lengo la kuimarisha mashirikiano ya kibiashara na maendeleo ya uchumi kwa maslahi ya nchini mbili.  


Katika mazungumzo yaliyofayika Kati ya ujumbe wa Tanzania na Muungano wa jumuiya za wenyeviwanda na Taasisi kuendeleza wazalishaji wadogo na wakati kwa nyakati tofauti ilibaanika kwamba pamoja na kwamba pamoja na Tanzania na brazil kushabihiana katika mazingira ya kijiografia , Mila na utamaduni ilibainika kwamba Tanzania ina fursa kubwa ya kujifunza kwa ndungu zao wa brazili hivyo wito ulitolewa wa kuwa na program za pamoja za mafunzo ya kujenga uwezo na kutembelea. 


Kwa upande wa utalii imebainika kwamba licha ya kuwa Brazil na Tanzania zina mazingira na vivutio vinavyolingana vya utalii  , brazili inapokea zaidi ya mara tatu ya idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania . Hivyo Tanzania ina mengi ya kujifunza kwa ndugu zao wa Brazil. Wito umetolewa kwa pande mbili kushirikiana kwa kubadilishana uzoefu, taarifa na utalamu pamoja na kutembelea na.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.