Habari za Punde

Watendaji wa Taasisi za Umma Watakiwa Kuacha Tabia ya Udokozi wa Vifaa Vinavyotolewa Msaada

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi akihakiki vifaa n a mashine zilizotolewa na Mfanyabiashara Said Bopar kabla ya kuvigawa kwa wahusika hapo Hospitali ya Abdullah Mzee Mkoa Kisiwani Pemba.
Balozi Seif akimpongeza Mzee Salum Abdulrahman Said aliyepatiwa Kigari kilihotolewa na Mfanyabiashara Said Nassir Bopar baada ya kukiangalia umadhubuti wake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi rasmi Kigari Mzee Salum Abdulrahman Said wa Mkoani Pemba ambae  ni mlemavu wa miguu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Biashara, Kiwanda cha Makonyo na Wizara ya Biahsra alipofika Kiwanda cha Makonyo Wawi kukagua Ujenzi wa Kiwanda Kipya kitachotumia mali ghafi ya Mkaratusi na Mlangilangi.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake chake Nd. Ramadhan Kombo Ferouz alimueleza Balozi Seif  mfumo wa uzalishaji katika Kiwanda Kikongwe cha Mafuta ya Makonyo.
Balozi Sdeif akiupongeza Uongozi wa Wizara ya Biashara na Viwanda kwa jitihada zake za kujenga Kiwanda kipya cha malighafi itakayotumia  Mkaratusi na Mlangilangi ambacho kitaongeza ajira.
Balozi Seif kati kati akimkabidhi Waziri wa Afya Mh. Hamad Rashid wa kwanza kulia Mashuka ya kulalia wagonjwa kwa Hospitali ya Vitongoji yaliyotolewa na Mfanya Biashara Said Nassir Bopar wa kwanza Kushoto.
Balozi Seif akimfariji Mtoto Mdogo aliyelazwa Hospitali ya Vitongoji akipatiwa matibabu mara baada ya kukabidhi msaada wa Vifaa kwa Hospitali hiyo.
Balozi Seif akimfanyia mzaha Mtoto Mdogo aliyelazwa Hospitali ya Vitongoji akipatiwa matibabu mara baada ya kukabidhi msaada wa Vifaa kwa Hospitali hiyo.
Mfanya Biashara Said Nassir Bopar akimpa Balozi Seif Mto na Kitanda kjukikabidhi kwa Uongozi wa Wizara ya Afya kwa ajili ya Hospitali ya Vitongoji.

Waziri wa Afya Zanzibar Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed akipokea msaada wa Sabuni kutoka Kwa Balozi Seif  yaliyotolewa na Mfanya Biashara Said Nassir Bopar.

Na.OthmanKhamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewatahadharisha Watendaji wa Taasisi za Umma wanaopata misaada na Vifaa kutoka kwa Wahisani kuacha tabia ya udokozi  wa vifaa hivyo unayoweza kupunguza nguvu za kuungwa mkono kwao.
Alisema vifaa na misaada hiyo lazima  isimamiwe katika kutoa huduma za muda mrefu, ambapo kinyume chake ni kuwavunja moyo wale wahisani na wafadhili wanaoamua kujitolea kusaidia Taasisi hizo.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Hospitali ya Vitongoji  na Abdullah Mzee wa Mkoani katika hafla ndogo ya kutoa msaada wa Vifaa mbali mbali kwa ajili ya matumzi ya Hospitali hizo na Sekta ya Kilimo vilivyotolewa na Mfanyabiashara Marufu Said Bopar kutekeleza ahadi aliyoitoa miezi michache iliyopita.
Alisema ipo mifano hai iliyowahi kutokea kwa baadhi ya Watendaji wakiwemo pia Viongozi wa Sekta ya Afya Nchini kujichukuliwa misaada na vifaa vilivyotolewa na Wafadhili pamoja na Wahisani udhaifu unaokera na kuchukiwa na Jamii.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimshukuru na kumpongeza Mfanyabiashara Said Bopar  kwa uzalendo wake wa Kusaidia zaidi Sekta za Elimu Kilimo pamoja na Afya maeneo muhimu yanayotowa huduma kubwa zaidi kwa Wananchi walio wengi hasa Vijijini.
Balozi Seif alisema wapo Wafanyabiashara wengine wenye uwezo mkubwa zaidi ya Bwana Bopar  ambao wana wajibu na stahiki ya kuunga mkono jitihada kama hizo ili Jamii iondokane na changamoto zinazoikabili ambazo zimo ndani ya mazingira ya Jamii yenyewe.
Akizungumzia stahiki za Wafanyakazi wa Sekta ya Afya hasa katika baadhi ya Hospitali ya Wilaya za Pemba Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikemea tabia ya baadhi ya Viongozi kuchelewesha Posho za Watendaji wao wanaowajibika hata katika muda wa ziada.
Alisema amekuwa akipokea malalamiko ya mara kwa mara wakati anapofanya ziara Kisiwani Pemba kutoka kwa Watendaji hao Hasa Hospitali ya Wete wakilalamikia kucheleweshewa Posho zao kwa zaidi ya Miezi Sita kitendo kinachowasikitisha na kuwavvunja moyo na yeye kumpa mashaka.
Balozi Seif  alionya kwamba hiyo wanayolalamikia kupewa sio bakhshish bali ni haki yao wanayostahiki kupewa  kuzingatia uwajibikaji wao unawalazimisha kufanya kazi katika muda wa ziada.
Halkadhalika Balozi Seif ameishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa moyo wake wa kusaidia huduma za Afya Visiwani Zanzibar tokea katika Miaka ya 60 kwa kuleta Mabingwa na Wataalamu wa Afya.
Wakati Serikali kupitia Wizara ya Afya ikijiandaa kukamilisha Jengo na Vifaa kwa ajili ya utoaji wa Huduma za maradhi ya Figo na Kisukari katika Hospitali ya Abdulla Mzee Mkoani juhudi zitafanywa za kuiomba China kusaidi mabingwa wa kutibu Maradhi ya Uti wa Mgongo.
Alisema maradhi maradhi ya Uti wa Mgongo hivi sasa yanaonekana kuongezeka kwa Kasi Kisiwani Pemba hali ambayo Serikali inalazimika kukabiliana nayo ili kuondosha hofu kwa Wananchi wake.
Mapema akikabidhi Vifaa na Msaada huo Mfanyabiashara Maarufu Nchini Bwana Said Bopar alisema  hiyo ni ahadi aliyoitoa kwa Uongozi wa Wizara ya Afya katika kusaidia changamoto zinazozikabili Hospitali mbali mbali hapa Nchini.
Bwana Bopar aliahidi kusaidia msaada wa chakula kwa Wagonjwa wote wanaolazwa katika Hospitali ya Vitongoji kwa kipindi cha Miezi sita kuanzia kipindi hichi.
Hatua hiyo ameichukuwa ili kuwapa faraja wagonjwa wote wanaopatiwa huduma za Afya kwenye Hospitali hiyo ili wajihisi kutotengwa na jamii katika kipindi wanachopata mitihani ya Maradhi.
Mfanya Biashara huyo katika msaada na vifaa hivyo alikabidhi Vitand 20 na Magodoro yake, Mashuka, Jiki, Utrasound ataipeleka Wiki ijayo pamoja na kusaidia Vitande vyengine 26 ili kuondosha kabisa upungufu wa vifaa hivyo katika Hospitali hiyo.
Pia akakabidhi mashuka 20, sabuni, viti vya kubebea wagonjwa kwa Hospitali ya Abdulla Mzee wa Mkoani shughuli iliyokwenda sambamba na kukabidhi mashine Nne za Kusagia nafaka, mbili za kusagia nyama pamoja na mashine Moja ya Juice ya Miwa kwa ajili  ya kusaidia Kituo cha kusarifu nafaka, Mabaraza la Vijana Chake na Mkoani pamoja na Jumuiya ya Wakulima Mkoani Kisiwani Pemba.
Akitoa shukrani Waziri wa Kilimo, Maliasi, Mifugo na Uvuvi Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri alisema Wizara hiyo itafuatilia vifaa vyote vilivyotolewa msaada ili vichangie kupunguza nguvu kubwa wanazotumia Wananchi hasa Wakulima katika kusarifu Mazao.
Waziri Mjengo alisema .Sekta ya Kilimo ni muhimu katika Uchumi wa Taifa na Ustawi wa Maisha ya Jamii kwani ndio chanzo cha chakula na takwimu zinaonyesha wazi kwamba Sekta hityo inachangia pato la Taifa kwa zaidi ya asilimia 20%.
Naye kwa upande wake Waziri wa Afya Zanzibar Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed aliwahakikishia Watendaji wa Wizara ya Afya madai ya malipo yao ya muda wa ziada yatazingatiwa na kutekelezwa mara tu baada ya kuingizwa fedha.
Waziri Hamad alisema Wizara ilichelewa kulipa malimbikizo hayo hasa kwa Hospitali ya Wete kutokana na uamuzi uliochukuliwa kwa agizo la Serikali la kulazimika fedha nyingi kuzitumia kwa wagonjwa waliopata rufa ya kupelekwa nje ya Nchi.
Baadae Balozi Seif aliyeambatana na baadhi ya Mawaziri alikagua maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Bohari Kuu ya Dawa Kisiwani Pemba linalojengwa pembezoni mwa Hsopitali hiyo ya Vitongoji.
Mkurugenzi Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar Bwana ZahranAli Hamad alimueleza Balozi Seif  kwamba ujenzi huo ulioanza Mwezi Mei Mwaka huu unatarajiwa kukamilika Mwezo Oktoba mwaka huu.
Bwana Zahran alisema ujenzi huo ulio chini ya usimamizi wa Wataalamu wa Wakala wa Majengo Zanzibarunatyarajiwa kugharimu jumla ya shilingi Bilioni 1.8 na kuchukuwa Miezi12.
Alisema kukamilika kwa Jengo hilo kutasaidia kuondosha usumbufu wanaoupata Watendaji wa Wizara ya Afya kupata huduma za Dawa kwa Bohamo Moja tuu Kua Maruhubi iliyopo Kisiwani Unguja.
Mapema asubuhi Balozi Seif alitembelea kiwanda cha Mafuta ya Makonyo kiliyopo Wawi Chake chake Pemba kujionea jengo jipya linalojengwa kukamua matufa yatayotokana na mali ghafi za Mkaratusi na Mlangilangi chini ya Kampuni ya Asian Roma ya China\.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Makonyo Nd. Ramadhan Kombo Ferouz alimueleza Balozi Seif  kwamba kiwanda hicho kitakapomaliza kujengwa kitachokuwa na vyungu Vitano kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mafuta ya Mimea yenye thamani ya shilingi Bilioni 10 kwa Mwaka.
Mkurugenzi Ramadhan alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba soko la bidhaa zitakazozalishwa na Kiwanda hicho kipya tayari limepatikana, kinachosubiriwa ni kuanza kazi mara ujenzi utakapokamilika Mwezi Oktoba Mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.