Habari za Punde

Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Ardhi na Mawasiliani Yatembelea Miradi ya Maendeleo Kisiwani Pemba

Mkurugenzi Mamkala ya Maji Kisiwani Pemba (ZAWA) Ndg.Omar Mshindo Makame akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya baraza la Wawakilishi katika kisima kinachudumia wananchi wa Mtambwe na Kisiwa Cha Kokota. 
Meneja wa Millelle Foundation Kisiwani Pemba Ndg.Abdalla Said Abdalla akieleza jambo mbele ya wajumbe wa kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya baraza la Wawakilishi kuhusiana na upelekaji wa maji safi katika Kisiwa Cha Kokota Wilaya ya Wete huko katika bandari ya Mkanjuni Mtambwe.
Waziri Maji Ardhi Nyumba na Nishati Zanzibar  Mhe.Salama Aboud Talib akizungumza na wajumbe wa kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya baraza la Wawakilishi pamoja na wananchi wa Kisiwa Cha Kokota baada ya kufanya ziara ya kutembelea Kisiwa hicho na kuangalia huduma ya maji safi
Mwenyekiti Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanziubar Mhe.Hamza Hassan Juma akizungumza na uongozi wa taasisi ya Millelle Foundation ambayo imesaidia katika kufikisha maji katika Kisiwa Cha Kokota Wilaya ya Wete huko Mkanjuni Mtambwe
Waziri Wizara ya Maji Ardhi Nyumba na Nishati Zanzibar Mhe.Salama Aboud Talib akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma, wakiangalia moja ya mifereji ya maji iliyowekwa na Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) katika Kisiwa cha Kokota Wilaya ya Wete Pemba, wakati wa ziara ya Kamati hiyo kutembelea Miradi ya Maendelo Kisiwani Pemba.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi wakionja ladha ya maji huko katika Kisiwa Cha Kokota Wilaya ya Wete.
Mwenyekiti  wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Hamza Hassan Juma akizungumza na wananchi wa Kisiwa Cha Kokota Wilaya ya Wete baada ya kufanya ziara kuangalia huduma ya maji safi na Salama.
Waziri wa Maji Ardhi,Nyumba na Nishati Zanzibar Mhe. Salama Aboud Talib akizungumza na wajumbe wa kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya baraza la Wawakilishi pamoja na wananchi wa Kisiwa Cha Kokota baada ya kufanya ziara ya kutembelea Kisiwa hicho na kuangalia huduma ya maji safi.

Baadhi ya Wananchi wa Kisiwa Cha Kokota Wilaya ya Wete wakiwasikikiza wajumbe wa kamati ya Ardhi na Mawasiliano ambayo ilifika Kisiwani huko kwa kuangalia maendeleo ya huduma ya maji safi na salama.
( Picha na Said  Abdulrahaman - Pemba.).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.