Habari za Punde

Kamati ya Maendeleo Wanawake Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Yakutana na Watendaji wa Wizara Vijana Sanaa na Michezo Zanzibar.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo Wanawake, Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi, Mwantatu Mbaraka Khamis, akifungua mkutano, wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo,kushoto Waziri wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe, Balozi Ali Karube na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Lulu Msham Abdallah. hafla  hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo
Katibu Mtendaji Baraza la Vijana Zanzibar, Khamis Faraji Abdalla, akisoma ripoti ya utekelezaji, kwa Kamati ya Maendeleo Wanawake, Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi, kwa Mwaka 2019 – 2020, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Sanaa Rahaleo
Mwakilishi wa nafasi za Wanawake, Sada Ramadhan Mwengwa, akiuliza maswali kwa Katibu wa Baraza la Vijana (hayupo pichani), wakati  Kamati ya Maendeleo Wanawake, Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi, ilipokutana na watendaji wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo hapo ukumbi wa Sanaa Rahaleo
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Amour Hamil Bakar, akijibu baadhi ya maswali yaliokua yakiulizwa na wajumbe wa Kamati ya Maendeleo Wanawake, Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi, hapo ukumbi wa Sanaa Rahaleo 
Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Ali Karume, akizungumza katika mkutano na wajumbe wa Kamati ya Maendeleo Wanawake, Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi, hapo ukumbi wa Sanaa Rahaleo
Watendaji wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika mkutano na wajumbe wa Kamati ya Maendeleo Wanawake, Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi, hapo ukumbi wa Sanaa Rahaleo (Picha na Abdalla Omar). 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.