Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Ujumbe wa Kampuni ya FCCPP

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya uzalishaji wa Umeme unaotumia Gesi ya Nchini Korea {FCCPP} Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.Kampuni hiyo imejizatiti kutumia fursa za Uwekezaji zilizopo Zanzibar kwa kutaka kuwekeza Mradi wao mkubwa utakaochangia Uchumi wa Taifa na kuongeza Mapato ya Nchi.Picha na – OMPR – ZNZ.                                                                                                                  

Na.Othman Khamis OMPR.
Uongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya uzalishaji wa Umeme unaotumia Gesi ya Nchini Korea {FCCPP}  imejizatiti kutumia fursa za Uwekezaji zilizopo Zanzibar kwa kuwekeza Mradi wao mkubwa utakaochangia Uchumi wa Taifa na kuongeza Mapato ya Nchi.
Mwakilishi wa Kampuni hiyo Profesa Injoon Suh alisema hayo wakati Timu yake ikitangaza nia yao ya kutaka Kuwekeza Mradi wao mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
Profeza Injoon Suh alisema Zanzibar imebarikiwa kuwa na Rasimlali nyingi za Uwekezaji ikiwemo mazingira bora ya hali ya Hewa inayowapa moyo wa kuanzisha Mradi wao unaokuwa ndani ya Bahari masafa ya Mita Mia moja umbali wa Ardhi unaoambatana na Mita Kumi Chini ya Bahari.
Alisema Umeme unaozalishwa na Kampuni hiyo unaweza kabisa kutumia Gesi Asilia inayozalishwa Nchini Tanzania kwa kuongezea na ile inayopatikana kutoka Mashariki ya Kati.
Profeza Injoon Suh alifahamisha kwamba kiwango cha Umeme utakaozalishwa na na Kampuni hiyo yenye uzoefu na Utaalamu wa masuala ya Nishati ya Gesi unafikia Mega Wats 215 kiwango ambacho ni kikubwa kwa Zanzibar kinachoweza kutosheleza mahitaji yote ya huduma hizyo.
Mwakilishi huyio wa Kampuni ya Kimataifa ya uzalishaji wa Umeme unaotumia Gesi ya Nchini Korea {FCCPP} alimuhakikishia Balozi Seif  kwamba Mradi huo una gerentii ya kufanya kazi katika kipindi cha Miaka 25 na baadae kukabidhiwa kwa Serikali.
Alieleza kwamba Kampuni ya FCCPP ni moja miongoni mwa Makampuni 15 yanayofanya kazi Kimataifa ndani ya Mwamvuli wa Kampuni ya Kitaifa ya Korea ya VOE Group.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema mradi wa uzalishaji wa Umeme wa kutumia Gesi Asilia alisema ni muhimu kwa vile umeonyesha muelekeo  kupungua kwa gharama za matumizi ya huduma hiyo.
Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bado ina nia ya kuwa na kianzio chengine cha Umeme utakaokuwa mbadala endapo hutokea hitilafu kwenye kianzio kimoja tu kilichopo kinachotumika hivi sasa Visiwani Zanzibar kilichoanzia Tanzania Bara.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushauri Uongozi wa Kampuni hiyo ya FCCPP kutoka Nchini Korea kutayarisha Maombi ya kuanzisha Mradi na kuyawasilisha Serikalini ili  kufanyiwa kazi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.