Na.Mwanajuma Juma.
TIMU ya soka ya Mboriborini imetwaa ubingwa wa bahari fm ndondo Cup kwa kuifunga pwani mchangani mabao 3-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa Amaan.
Fainali hiyo ya aina yake imechezwa saa 10:00 za jioni na kuhudhuriwa na mashabiki wengi waliovutia uwanja mzima.
Katika mchezo huo ambao mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Katibu mkuu uvccm Zanzibar Mussa Haji Mussa Mboriborini mabao yake yote hayo yalifungwa na Said Etoo.
Mshindi wa kwanza wa michuano hiyo aliondoka na shilingi milioni tatu, Kombe jezi na mpira, wa pili alipata shilingi milioni moja na nusu, jezi na mpira na mshindi wa tatu aliondoka na kitita Cha shilingi milioni moja na mpira.
Aidha zawadi ya Kipa Bora ilikwenda Sheha Kirara kutoka timu ya Pwani Mchangani , mchezaji Bora Ridhwani Mohammed wa Mboriborini na mfungaji Bora ni maulid wa Chaani Masingini kashinda magoli sita.
Kwa upande wa zawadi ya Timu yenye nidhamu ilikwenda Six Center ya Mwera .


No comments:
Post a Comment