Habari za Punde

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Ritta Kabati Atimiza Ahadi Yake ya Kukarabati Shule ya Msingi Kihesa

Diwani wa kata ya Kihesa Ndg.Jully Sawani akiongea na mwandishi wa habari ofisini kwake

Na. Fredy Mgunda -Iringa.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati ametakiwa kutimiza ahadi ya kukarabati shule ya msingi Kihesa kama alivyowaahidi wakazi wa kata ya kisheza wakati wa mkutano wa hadhara uliyofanyika katika shule hiyo.

Akizungumza na blog diwani wa kata ya Kihesa Jully Sawani amemuomba mbunge huyo kutimiza ahadi aliyoitoa kwa lengo la kuhakikisha wanaboresha sekta ya elimu katika kata hiyo.

“Naomba nimpongeze bwana Jose Mgongolwa kwa kusaidia kukarabati baadhi ya majengo ya madarasa kwa msaada wake wa kukarabati madarasa hayo katika shule ya msingi Kihesa” alisema Sawani

Kwa upande wake Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati amesema kuwa atatimiza ahdi hiyo mwezi wa tisa akitoka bungeni na kila kitu kipo sawa.

“Utaratibu wa sasa ukiomba pesa kwa wadau unatakiwa kutoa account ya Halmashuri ili kila kitu kinapitia kwenye ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri hivyo tayari wadau tayari wameshazitoa na zipo halmashuri” alisema Kabati

Aidha Kabati amesema anamifuko ya saruji zaidi ya mia saba kwa lengo la kukamilisha ahadi zote alizoahidi katika shule mbalimbali mkoani Iringa.

Mwezi wa tisa naanza kutekeleza ahdi zote kwa kuwa pesa ninazo hivyo ni jukumi la mkurugenzi kuninunulia mifuko hiyo ya sariji ili nianze kutimiza ahadi zote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.