Habari za Punde

Mfumko wa Bei Umepungua Kwa Asilimia 2.4 Kulingana na Mwezi wa Juni 2019.

Mkuu wa Kitengo cha Takwim na Bei, kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Khamis Abrahmani Mshamu akielezea juu ya kushuka kwa mfumko wa bei kutoka mwezi wa sita 2019 ulikuwa asilimia 2.7 ikilinganishwa na asilimia 2.4 kwa mwezi wa saba 2019.
Mkuu wa Kitengo cha Takwim na Bei, kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Khamis Abrahmani Mshamu akielezea juu ya kushuka kwa mfumko wa bei kutoka mwezi wa sita 2019 ulikuwa asilimia 2.7 ikilinganishwa na asilimia 2.4 kwa mwezi wa saba 2019.
Baadhi ya wandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali na Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakisikiliza tarifa ya kushuka kwa bei kutoka mwezi kwa mtakwimu mkuu.
Mhadhiri Mkuu Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) Dr. Suleiman Simai Msaraka akielezea hali ya uchumi na kushuka kwa bei kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati wakati wa mkutano na wandishi wa habari uliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Mazizini Mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga.

Na Mwashungi Tahir - Maelezo. 
Afisi ya Mtakwim Mkuu wa Serikali Zanzibar imesema hali ya mfumko wa bei kwa mwaka uloishia Julai 2019 umepungua kwa asilimia 2. 4 ukilinganisha na 2. 7 mwaka ulioishia June 2019.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Takwimu za bei kutoka afisi ya Mtakwimu Mkuu   Khamis Abdulrahman Msham amesema kupungua kwa bidhaa hizo zimetokana  na kwa baadhi ya bidhaa mbalimbali zikiwemo chakula petrol bidhaa nyengine za matumizi ya mwanaadam.

Amesema kushuka kwa mfumo wa bei   kwa bidhaa muhimu kumetokana na ongezeko la uzalishaji na kuweza  kufanya bidhaa kushuka.

Nae Mkuu wa Idara ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu Zanzibar SUZA Dk Suleiman Simai Msaraka àmesema kupungua kwa bidhaa hizo  kutokana na hali ya uzalishàji mzuri wa bidhaa za vyakula kwa maeneo husika.

Amefahamisha kuwa hali haiko vibaya kutokana na kuwa  bidhaa zipo za kutosha kuwafikia mahitaji kwa walaji hivyo amewataka wananchi kuongeza uzalishaji ili mfumo wa bei uweze kushuka.

Pia ameeleza kwamba kutokana na usimamizi mzuri Bank of Tanzania  pamoja na Wizara ya Fedha kwa kusimamia vizuri mfumko wa bei kwa bidhaa muhimu kwa maisha ya wanaadamu.

Kwa upande wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Zanzibar ZURA Uchumi na Masoko Omar Ali Yussuf amesema sekta zote zinategemeana hivyo kwa upande wa suala la mafuta ni muhimu sana kwani uchumi pia unaongezeka .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.