Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein Azungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.

 Baadhi ya  Viongozi mbali mbali katika   Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale  wakisimama wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)  alipoingia katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar kabla kuanza  Mkutano wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 uliofanyika leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisisitiza jambo wakati alipokuwa  akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale katika mkutano wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale anayeshuhulikia Habari Dkt.Saleh Yussuf  Mnemo (wa pili kushoto) akitoa ufafanuzi  wakati wa Mkutano wa Wizara hiyo  wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale anayeshuhulikia Utalii na Mambo ya kale Dkt .Amina Ameir Issa (kushoto) na kulia Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndg. Omar Said Ameir.
Baadhi ya Maafisa katika Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale  wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza na Ungozi wa Wizara hiyo leo katika  Mkutano wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar. 
[Picha na  Ikulu.] 22/08/2019.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.