Habari za Punde

Serikali Inatekeleza Miradi ya Ujenzi wa Madampo ya Kisasa Nchini Kuwezesha Wananchi Kupata Eneo la Kutupia Taka Ngumu.


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jafo akizungumza wakati wa ziara yake kwenye dampo la Kisasa la Jiji la Tanga kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jafo amesema serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa madampo ya kisasa kwenye majiji mbalimbali hapa nchini ili kuwezesha wananchi kupata eneo la kutupia taka ngumu ambazo zimekuwa zikizalishwa. 


Aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga ambapo pia alitembelea dampo la kisasa linalojengwa eneo la Mabokweni Jijini humo huku akionyeshwa kuridhishwa na ujenzi huo.

Alisema madampo hayo ya kisasa yatakuwa na msaada mkubwa ya kuondosha changamoto ya taka ngumu ambazo zinazalishwa kwenye maeneo mbalimbali na kukosa eneo la kuhifadhi

“Madampo haya yamekwisha kujengwa na kukamilika majiji nchini likiwemo Jiji la Arusha lengo likiwa kuhakikisha taka ngumu zinazozalishwa ziweze kufika eneo la dampo lililokuwa sahihi zaidi”Alisema Waziri Jafo.

“Kwa kweli niwashukuru Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji umekuwa wa mfano nchi nzima pamoja na watendaji wako na madiwani mmefanya kazi kubwa na nzuri sana huwaga sipendi kusifu vitu vya hovyo lakini kwa hili mnastahili Pongezi”Alisema

“Sipendi kusifu vitu vya hovyo lakini Tanga jiji mnastahili Pongezi mmetoa fedha bilioni 6 kwa ajili ya mradi huu mpaka sasa kati ya Bilioni 9 niwapongeze dampo hili ni la kipekee ambalo lenye ekari 75 zote mmeliwekea ukuta wa kisasa kama ule wa mererani wengine wachovu hawawezi kufanya hivyo”Alisema

Waziri huyo aliwataka viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam waenda kujifunza Tanga ili waone namna wanavyotekeleza miradi iliyopo kwenye maeneo yao na kuweza kuleta tija kubwa na ufanisi kama ulivyokuwa mradi huo.

“Tunataka wengine waige utendaji wa Jiji la Tanga Mkurugenzi Mayeji wewe ni mkurugenzi Supa sana ...Jiji la Dar es Salaam tumewapa fedha kwa ajili ya ujenzi wa machinjia vingunguti,soko la magomeni,soko la kisutu,kuimarisha ufukwe wa coco beach lakini hata hizo ambazo zimefanyika ni kwa ajili ya mikimiki watu wanataka mpaka Waziri uenda ndio watekeleze”Alisema

Aidha alisema hiyo sawa kabisa lazima viongozi waliopewa dhamani ya kusimamia mikoa, wilaya kila huku akieleza kwamba haipendezi mpaka waziri aende akasimamie mchakato wa manunuzi.

“Leo Dar kila mradi lazima watu wagombane ujenzi wa stendi ya Mbezi Luis watu wanaogomba jinsi ya kumpata nani mkandarasi ili aweze kujenga..leo hii pale Coco Beach watu wanagombania ni ubabaishaji tu kila mtu anakuja na mkandarasi wake mkononi lakini Tanga ukija kila mradi umesimaia vizueri”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba Mkurugenzi Jiji la Tanga umekuwa wa mfano bora wa kuigwa yeye na  watendaji wake ,meya na baraza la madiwani wa Tanga ni la mfano wea kuigwa kwenye maeneo mengo kwa maana mnatekeleza wajibu wenu ipasavyo.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jafo  katikati akitembelea dampo la kisasa la Jiji la Tanga leo wakati wa ziara yake kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jafo kushoto  akitembelea dampo la kisasa la Jiji la Tanga leo wakati wa ziara yake kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akifuatiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
 Muonekano wa dampo la kisasa la Halmashauri ya Jiji la Tanga



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.