Habari za Punde

Ufunguzi wa Kongamano la Biashara Kati ya Tanzania na Uganda Lafanyika Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashingwa akifunga kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania Septemba 6-7, 2019 ambapo Kongamano hilo liliwahusisha wafanyabishara wa nchi zote mbili na yalifunguliwa Septemba 6, 2019 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Picha zote  na Matokeo Chanya+
Wafanyabiashara wa Tanzani na Uganda wakifuatilia.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Edwin Rutageruka akielezea mambo machache wakati wa kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania Septemba 6-7, 2019.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashingwa (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (kushoto) wakifuatilia kwa makini.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bwana Godfrey Simbeye.
Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wakifuatilia tukio hilo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bwana Godfrey Simbeye akihutubia wakati wa ufungaji wa kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania Septemba 6-7, 2019 ambapo Kongamano hilo liliwahusisha wafanyabishara wa nchi zote mbili na yalifunguliwa Septemba 6, 2019 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.  
Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wakifuatilia tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.