Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi
Joseph Sokoine akiwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Abdallah Hassan Mitawi, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ofisi
za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar hiyo Mhe. Ali
Selemani Ali na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais
Lupi Mwaikambo wakiwa katika eneo la kiwanja kilichokabidhiwa kwa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar.
Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi
Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wametembelea kiwanja kwa
ajili ya kujengwa Ofisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) katika eneo
la Mahoma Makulu Jijini Dodoma.
Ziara hiyo pia ilihusisha wataalamu kutoka
Serikali hiyo na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Zanzibar Mhe. Mihayo Juma Nhunga ambaye aliishukuru Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa kuwakabidhi pa kiwanja hicho.
Mhe. Nhunga alisema kuwa SMZ inafarijika kupata
kiwanja hicho ambacho kina ukubwa wa hekta 30 na kuwa itaanza haraka ujenzi wa izo
uhusiano wa pande mbili za Muungano utaendelea kuimarika.
Serikali hizi mbili zina uhusiano na ushirikiano
mzuri na tunaona namna Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilivyojitoa na kutupatia
kiwanja hiki na tunaona thamani ya Dodoma sasa tofauti na zamani hivyo tunaanza
haraka ujenzi wa ofisi zetu tuhamie hapa," alisema.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo
Mhe. Ali Selemani Ali wanashukuru kwa kupata ardhi hiyo na kuwa ina thamani
kubwa kwa Serikali ya Zanzibar hivyo undugu baina ya pande hizo mbili
utaendelea kuimarika.
Mhe. Ali aliahidi kuwa kama Kamati wataishauri
SMZ kuanzisha ujenzi wa Ofisi za serikali hiyo kwa kasi ili waweze kuhamia na
kuanza shughuli zake katika Jiji la Dodoma.
Akitoa shukrani zake kwa ujumbe huo Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine aliyeambatana na wakurugenzi
wa Idara ya Muungano aliwakarisha kuanza
ujenzi na kuhamia.
Balozi Sokoine alisema kuwa kukamilika kwa
ujenzi wa Ofisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutaimarisha Muungano na
undugu baina ya wananchi wa pande hizo mbili.
"Tunafarijika sana tunapoona mnafika hapa
kwenye kiwanja chenu mara kwa mara na kuona namna mtakavyoanza ujenzi na
kukamilika kwa Ofisi hizi kutaleta ushirikiano mzuri baina yetu sote,"
alisema.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Zanzibar
Mhe. Mihayo Juma Nhunga akizungumza wakati wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi
za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar
walipotembelea eneo la kiwanja walichokabidhiwa SMZ na Serikali ya Muungano.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ofisi
za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar hiyo Mhe. Ali
Selemani Ali akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati hiyo na viongozi mbalimbali
walipofika katika eneo walilokabidhiwa.
Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi
Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wakikagua eneo
walilokabidhiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Wajumbe wakiangalia ramani ya eneo hilo
walilokabidhiwa kutoka kwa mtaalamu wa ardhi.
No comments:
Post a Comment