Habari za Punde

Balozi Seif akutana na Ujumbe wa Viongozi Waandamizi wa Chuo Kikuu cha Al – Azhar cha Nchini Misri

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Viongozi Waandamizi wa Chuo Kikuu cha Al – Azhar cha Nchini Misri ulioongozwa na Sheikh Saleh Abbas Goma ambae ni Katibu wa Saleh Grand ya Imam wa Chuo Hicho.  
 Kiongozi wa Ujumbe wa Viongozi Waandamizi wa Chuo Kikuu cha Al – Azhar cha Nchini Misri Sheikh Saleh Abbas Goma ambae ni Katibu wa Saleh Grand ya Imam wa Chuo akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Balozi Seif.
 Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watui {UNFPA} Bibi Jacqueline Mahon akielezea nia ya Shirika lake kuendelea kuiunga Mkono Tanzania katika Taaluma ya Ulezi wa Familia
 Baadhi ya Viongozi Waandamizi wa Chuo Kikuu cha Al – Azhar cha Nchini Misri wakifuatilia mazungumzo yao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Balozi Seif akipokea zawadi ya Vitabu mbali mbali kutoka kwa Ujumbe wa Viongozi Waandamizi wa Chuo Kikuu cha Al – Azhar cha Nchini Misri.
Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kila Mtoto katika Dunia hii ana haki ya kuishi, kuhudumiwa, kupata Elimu na pamoja na Uhuru wa Kibinaadamu, na hili litapatikana kama Jamii iliyomzunguuka itaendelea kuzingatia Uzazi wa Mpango.
Alisema masuala ya Uzazi wa Mpango pia yanakubalika ndani ya Dini pamoja na madhehebu tofauti yanayoelekeza Familia kumnyonyesha Mtoto kuanzia siku Moja hadi Miaka Miwili ili kukamilisha Haki yake ya kupata virutubisho kutoka kwa Mama Mzazi.
Balozi Seif Ali Iddi akitoa kauli hiyo Ofisini kwake Vuga wakati wa mazungumzo yake na Viongozi Waandamizi wa Chuo Kikuu cha Al – Azhar cha Nchini Misri ulioongozwa na Sheikh Saleh Abbas Goma ambae ni Katibu wa Saleh Grand ya Imam wa Chuo Hicho.
Ujumbe huo upo Tanzania kwa mwaliko wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu {UNFPA} chini ya Mwakilishi Mkaazi wake Nchini Tanzania Bibi Jacqueline Mahon.
Balozi Seif alisema Familia zinapaswa kuendeshwa kwa kutumia mfumo uliokubalika ndani ya Vitabu vya Dini ambavyo tayari vimeshatoa muelekeo wa Malezi ya Kifamilia yanayokubalika hata kwenye mfumo wa kisasa wa kujali kukitunza Kizazi.
“ Uzazi wa mpangilio umekubalika ndani ya Dini ya Kiislamu na ndio ikasisitizwa Mtoto anyonyeshwe Miaka Miwili ili kutoa muda kwa Mtoto mwengine kupata Haki yake ya Msingi”. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushukuru Uongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu {UNFPA} kwa jitihada zake za kuiunga Mkono Tanzania na Zanzibar katika masuala ya Malezi ya Watoto ndani ya Familia za Wananchi walio wengi Nchini.
Mapema Kiongozi wa Ujumbe huo wa Viongozi Waandamizi wa Chuo Kikuu cha Al – Azhar cha Nchini Misri Sheikh Saleh Abbas Goma ambae ni Katibu wa Saleh Grand ya Imam wa Chuo Hicho alisema Uislamu muda wote unazingatia na  kusisitiza uwepo wa Jamii yenye Afya na Nguvu.
Sheikh Saleh Abbas Goma alisema Maandiko Matukufu ya Quran yanampa Muumini aliyeamini Kitabu hicho muongozo wa maisha yake ya kawaida yanayompa fursa  ya kuishi kwa upendo na Taqwa.
Naye kwa upande wake Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watui {UNFPA} Bibi Jacqueline Mahon alisema masuala ya Idadi ya Watu na namna ya Maisha yao yameshazungumzwa na kuandikwa katika Vitabu mbali mbali Duniani.
Bibi Jacqueline Mahon alisema Taasisi hiyo kupitia Wataalamu wake itaendelea kubeba jukumu la kutoa Taaluma kwa Taasisi na Mataifa mbali mbali Ulimwenguni ili kuona uwepo wa Idadi ya Watu Duniani inakwenda sambamba na ukuaji wa Uchumi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.