Mnyama aina ya Punda ambaye anapiganiwa kupata haki na sheria zake na Shirika la Inades Formation Tanzania (IFTz)
Na.Fredy Mgunda.Iringa.
Shirika la Inades Formation Tanzania (IFTz) limeitaka jamii kutambua haki na sheria za mnyama punda pamoja na kutambua mchango wa punda katika maisha ya jamii.
Akizungumza na vyombo vya habari mratibu wa kuboresha maisha kupitia ustawi wa mnyama kazi punda Fadhili Nyingi ambapo amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuboresha maisha ya watu waishio vijijini kupitia mnyama punda pamoja na kurasimisha sekta ya punda katika halmashauri ya wilaya ya iringa.
Lengo la kwa la mradi ni kuongeza uelewa wa watu juu ya haki za wanyama na ufugaji bora wa Punda,mwisho wa siku watu wanatakiwa kujua punda anatakiwa kula nini,analala wapi na anahaki gani za msingi kutoka kwa binadamu” alisema Nyingi
Nyingi alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaongeza uelewa kwa wananchi juu ya mnyama punda na kuwa sekta rasmi kama zilivyo sekta nyingine.
Aidha ameeleza mafanikio waliyopata kutokana na mradi huo ikiwa ni pamoja na kubadili mitizamo ya wananchi na kupunguzwa ukatili dhidi ya mnyama punda.
“Mafanikio yapo toka tumeanza mradi huu,maana wananchi wengi waliopo vijijini wameanza kubadilika kimtadhamo juu ya mnyama punda ndio maana sasa wameanza kuacha kuuza punda” alisema Nyingi
Kwa upande wake afisa mfawidhi nyanda za juu kusini bwana Nong’ona Solomoni amebainisha baadhi ya magonjwa yanayokumkumba mnyama punda ni pamoja na pepo punda,homa ya farasi na vidonda.
Hata hivyo kupitia mradi huo wa Inades Formation Tanzania wamefanikiwa kuunda vikundi 6 vya kukopeshana pamoja kutoa elimu juu ya haki za wanyama.
No comments:
Post a Comment