Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba.Mwalimu.Mohammed Nassor
Salim akifungua mkutano wa mafunzo kwa Walimu wa Somo la Kiswahuili Kisiwani Pemba yaliofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Walimu TC Michakaeni mafunzo hayo yamefanyika leo.
Na Ali.Othman - Pemba.
Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Ndg.Mohammed Nassor
Salim amewataka walimu wa somo la Kiswahili kisiwani Pemba
kutumia kipindi kifupi kilichobaki kuwaandaa wanafunzi katika mbinu bora
za kujibu maswali ya somo hilo.
Mw.Mohammed ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa walimu wa somo la Kiswahili
yaliyoandaliwa na Idara ya Mafunzo ya uwalimu katika ukumbi wa TC Michakaeni Pemba leo.
Amesema ipo haja kwa walimu wa somo la Kiswahili kuunda umoja na kufanyakazi kwa bidii ili kukuza ufaulu wa somo hilo kwa wanafunzi na kuimarisha hadhi ya Kiswahili
visiwani Zanzibar.
Awali, Mkurugenzi Idara ya Mafunzo ya Ualimu Bi.Maimuna Fadhili
Abass amesema Idara yake imeamua kufanya mafunzo hayo baada ya kubaini kwamba ufaulu wa somo
la Kiswahili hauridhishi kulingana na hadhi ya Kiswahili Zanzibar.
‘’Tuliamua kuandaa mafunzo haya baada ya kukaa na washauri wa somo la Kiswahili na kutathmini hali ya matokeo ambapo tuliona hayaridhishi hasa katika mada za uandishi, fasihi na sarufi’’ Amesema Bi Maimuna.
Aidha Bi.Maimuna amesema mafunzo hayo yatasaidia kuwaweka pamoja walimu wa somo la Kiswahili na kuunda umoja utakaowasaidia kujadili mada mbali mbali na kutatua changamoto zinazowakabili katika ufundishaji wa somo hilo.
Nae Mratibu Idara ya Mafunzo ya Uwalimu Mw.Hemed Said Masoud ameishukuru Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kupitia Idara ya Mafunzo ya Ualimu kwa kuandaa mafunzo hayo ambapo amewataka walimu kutumia kipindi kifupi kilichobaki kuwaandaa wanafunzi waweze kufaulu kwa kiwango kilicho bora Zaidi.
Mafunzo kama hayo yalifanyika Kisiwani Unguja mnamo mwezi wa 8
(August) mwaka huu ambapo walimu wasomo hilo walipata fursa ya kujumuika na kujadili changamoto mbali mbali zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.
MkurugenziIdarayaMafunzoyaUalimu Bi MaimunaFadhili Abas
akimkaribishaAfisaMdhaminiWizarayaElimunaMafunzoyaAmali Mw. Moh’dNassor Salim
katikaufunguziwamafunzoyasikutatukwawalimuwasomo la Kiswahili katikaukumbiwa TC
Michakaeni.
WalimuwaSomo la Kiswahili waSkulimbalimbalizaMkoawaKusini
Pemba wakiwakatikaUkumbiwa TC MichakaenikatikaUfungunziwaMafunzoyasikutatuyaliyoandaliwanaIdarayaMafunzoyaUalimu.
No comments:
Post a Comment