Habari za Punde

Balozi Seif Anatarajiwa Kuyafungua Mashindano yaMapinduzi Cup Kwa Mashirika ya Serikali na Wizara Kuadhimisha Sherehe za Mapinduzi

Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Omar Hassan Omar akizungumza na Waandishi wa Habari huko Ofisini kwake Migombani Mjini Unguja kuhusu mashindano ya Mapinduzi CUP ya Wizara , Taasisi na Mashirika ya Serikali yatayoanza  18 mwezi huu. .
 Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Omar Hassan Omar akizungumza na Waandishi wa Habari huko Ofisini kwake Migombani Mjini Unguja kuhusu mashindano ya Mapinduzi CUP ya Wizara , Taasisi na Mashirika ya Serikali yatayoanza 18 mwezi huu. .
Baadhi ya Waandishi wa Habari Wakimsikiliza   Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Omar Hassan Omar akielezea  kuhusu mashindano ya Mapinduzi CUP ya Wizara , Taasisi na Mashirika ya Serikali  yatayoanza tarehe 11 mwezi huu. hafla iliyofanyika .Ofisini kwake Migombani Mjini Unguja.
Picha na Maryam Kidiko - Maelezo Zanzibar..

Na Habari  Maelezo.
Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi anatarajiwa kuyafungua Mashindano ya Mapinduzi Cup ya Mawizara,Taasisi na Mashirika ya Serikali tarehe 18/12/2019 huko katika Uwanja wa Mou-Tse -Tung.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Katibu Mkuu Wizara ya Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo Hassan Omar Hassan (Kingi) amesema kuwa mashindano hayo yanalengo la kuongeza hamasa katika michezo ndani ya Taasisi.
Amesema katika kutekeleza tamko la sera ya michezo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya kushiriki michezo hiyo kuipa kipaumbele katika taasisi za elimu pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama.
Aidha amesema kuwa michezo hiyo itakuwa endelevu kwa taasisi za SMZ na SMT  na itashirikisha wafanyakazi wa kudumu wa taasisi hizo na asiwe muajiriwa wa mkataba au wa kutwa.
Aidha Kingi amesema ili kuhakikisha kuwa washiriki wa mashindano hayo pia atawasilisha kitambulisho chake cha kazi chenye picha yake na sahihi ya mechi atakayocheza.
Hata hivyo alisema kuwa mshiriki atawasilisha jina kamili ya nambari ya ajira pamoja na cheo chake na kituo chake cha kazi.
Vilevile ameeleza kuwa mashindano hayo hayatahusisha wachezaji wanaocheza ligi kuu na madaraja ya kwanza ya michezo husika.
Pamoja na hayo amefafanua kuwa michezo ambayo imethibitishwa ni mpira wa miguu, riadha, kuvuta kamba,,,netball,,,bao, ,karata,,draft,,table tennis pamoja na nage.
Vilevile alisema kuwa michezo hiyo itachezwa katika viwanja vya Amani,KMKM  pamoja na Mou wakati wa asubuhi na jioni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.