Habari za Punde

Katibu Mkuu Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Ndg. Omar King Azungumza na Viongozi wa Wasanii wa Wilaya za Unguja

Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Omar  Hassan King akizungumza na Viongozi wa Wasanii wa Maigizo kutoka Wilaya zote za Unguja, Kikao kilichofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzuibar.
Mjumbe wa Bodi ya Wasanii Zanzibar Mussa Makame Pandu akitoa maelezo kwa Viongozi wa Wasanii (hawapo Pichani)  katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo.
Baadhi ya Viongozi wa Wasanii  wa Maigizo kutoka Wilaya zote za Unguja wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Omar Hassan King (hayupo pichani)  katika Kikao cha Viongozi hao kilichofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo.
Picha Na Maryam Kidiko - Maelezo Zanzibar.

Na Kijakazi Abdalla - Maelezo  Zanzibar.
WASANII wa Sanaa za maigizo Zanzibar wametakiwa kuzisajili kazi zao katika Ofisi ya Msajili wa Hakimiliki Zanzibar (COSOZA) ili kuzilinda na kupata haki stahiki zao.
Akizungumza katika kikao cha Viongozi wa Wasanii wa maigizo Katibu Mkuu Wizara ya Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo Omar Hassan (Kingi) huko katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Amesema iwapo wasanii kazi zao hawatozisajili katika taasisi hiyo itakuwa vigumu kwa taasisi kuwa na  nguvu ya  kuweza kuzitetea kazi zao na kupata haki stahiki.
Amesema kumekuwepo na malalamiko ya wasanii kukosa haki zao hii inatokana  wasanii kutojisajili katika ofisi hizo  na kushindwa kuzitambua kazi zao
Aidha Katibu Kingi amesema kuwa Sanaa ya maigizo Zanzibar imeshuka hivyo ipo haja ya kuchukuwa juhudi ya kuhakikisha Sanaa hiyo inakuwa kwa kasi kubwa na kuweza kulinda maslahi yao.
Amesema kuwa katika kuitambua suala hilo Wizara imeweza kuchukua hatua ya kuratibu wasanii kila wilaya  ili  kuwatambua umuhimu wao katika kazi zao  pamoja na kuwaengezea kipato.
Vilevile amesema kuwa ipo haja wasanii wa Zanzibar kuzirejesha Sanaa za maigizo ya kizamani ili kuweza kulinda mila silka na utamaduni wa visiwa hivi jambo ambalo linaonekana kutoweka.
Hata hivyo amewataka wasanii wa Zanzibar kuwa na umoja wa wasanii ili kuwatambua wasanii wa zamani na wapya ambao wanachipukia katika kazi hiyo.
Amesema kuwa hivi sasa wasanii wa Zanzibar wamekuwa hawana umoja  jambo ambalo limekuwa vigumu kuweza kuwasaidia pale inapotokea wanahitaji misaada ya kiserikali.
Aidha amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wasanii wa Zanzibar wanafaidika na kazi zao kwa kuutambua mchango wao waliotoa katika kazi ya tasnia hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.