Habari za Punde

Takwimu za Matukio ya Ajali za Barabarani Mwezi wa Novemba 2019.

Mtakwimu kitengo cha makosa ya jinai, madai na jinsia kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar Asha Mussa Mahfoudh (wa pili kutoka kulia) akitoa takwimu za ajali na makosa ya barabarani kwa mwezi wa Novemba mwaka 2019 kwa wandishi wa habari wa vyomba mbalimbali, hafla iliyofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serekali ya Zanzibar iliyopo Mazizini Mjini.
Mkuu wa Kitengo cha Takwimu za uhalifu Makao Makuu ya Polisi Zanzibar, Mkaguzi wa Polisi Khamis Mwinyi Bakari akijibu maswali yaliyoulizwa na wandishi wa habari katika mkutano wa takwimu za ajali na makosa ya barabarani uliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serekali Zanzibar. (Kulia) Mkuu wa Kitengo cha makosa ya jinai, madai na jinsia Ofisi ya Mtakwimu Zanzibar Bi. Mwanajuma Ali Suleiman.
Baadhi ya wandishi wa habari wakifuatilia tarifa ya takwimu za ajali na makosa ya barabarani zilizotolewa na Mtakwimu kitengo cha makosa ya Jinai, madai na jinsia kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar Asha Mussa Mahfoudh (hayupo pichani).
Mwandishi wa habari Kauthar Abdalla wa Gazeti la Zanzibar leo akiuliza swali katika Mkutano wa takwimu za ajali na makosa ya barabarani kwa mwezi Novemba mwaka 2019.
Na.Mwashungi  Tahir  Maelezo Zanzibar.
Jumla ya ajali  za barabarani33 zimeripotiwa mwezi wa Novemba 2019 ambapo waathirika 105 kati ya hao 64 walikuwa wanaume na 21 ni wanawake miongoni mwao waliokufa ni 12 na waliojeruhiwa ni 93.
Ameyasema hayo Asha Mussa Mahfoudh Mtakwimu kutoka kitengo cha makosa ya jinai, madai na jinsia wakati alipokuwa akiwasilisha takwimu za ajali na makosa ya barabarani  kwa waandishi wa habari  huko kwenye Ukumbi  wa Mtakwimu Mkuu uliopo Mazizini.
Alisema  makundi yaliyoathirika katika ajali hizo ni pamoja na waendao kwa miguu, madereva, wapanda baskeli na pikipiki pamoja na abiria.
Pia amesema mlinganisho wa idadi za ajali kwa mwezi uliopita zimeongezeka kutoka ajali 32 kwa mwezi wa Oktoba , 2019 hadi 33 mwezi wa Novemba 2019.
Kwa upande wa makosa ya barabarani amesema jumla ya makosa 1, 553 yameripotiwa mwezi wa Novemba 2019 ambapo makosa hayo yamefanywa na wanaume.
Alisema Wilaya ya Mjini, Magharibi “A” na Magharibi “B” zinaongoza zaidi kwa makosa ya kushindwa kuvaa sare na beji kwa utingo na dereva wa gari za abiria , kutofuata miongozo na kanuni za usalama barabarani.
Aidha amesema makosa mengine ni pamoja na kuendesha chombo cha moto bila ya leseni, bima na leseni ya njia, kuendesha chombo cha moto bila ya kuvaa  helment na kuzidisha idadi ya abiria na mizigo.
Nae Mkaguzi wa Polisi Khamis Mwinyi Bakari amesema ongezeko la ajali kwa Wilaya ya Magharibi B linasababishwa na ubovu wa barabara na pia ajali nyingi husababishwa na uzembe wa madereva  na mwendo kasi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.